Asasi
ya Kijamii ya Catherine Foundation jana imetembelea kituo cha kulelea wa
watoto cha Matumaini Village kilichopo mkoani Dodoma ambapo walikwenda
kutoa misaada mbalimbali wakiongozwa na Mkurugenzi wa Asasi hiyo,
Catherine Magige.
Katika
Hafla hiyo Mgeni Rasmi alikuwa Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda
ambapo asasi hiyo ilitoa vitu mbalimbali vikiwemo, Madaftari, Mafuta,
Sabuni, Juice, miswaki na dawa zake, mchele, sukari, nguo za watoto,
kanga za wakinadada wanaowalea watoto hao na vingine vingi.
Mama Tunu Pinda akihutubia
Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda akihutubia katika hafla hiyo.
Mkurugenzi wa Catherine Foundation, Mhe Catherine Magige akihutubia katika hafla hiyo
Mkurugenzi
wa Catherine Foundation, Catherine Magige akizungumza na watoto
wanaolelewa kwenye Kito cha Matumaini Village kilichopo Dodoma
alipokwenda kutoa msaada
Mhe Catherine Magige akicheza na mmoja wa watoto wa kituo hicho
Mkurugenzi
wa Catherine Foundation, Mhe Catherine Magige akiwa na mtoto mchanga
anaye lelewa katika Kituo cha Matumaini Village mjini Dodoma jana.
Mke
wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda na Mkurugenzi wa Catherine Foundation,
Mhe Catherine Magige wakizungumza na watoto wanaolelewa kwenye kituo
hicho.
Mama Tunu Pinda na Mhe Catherine Magige wakiwa na watoto hao
Mama Tunu Pinda akikabidhi zawadi mbalimbali zilizotolewa na asasi hiyo
Misaada mbalimbali ikitolewa
Mkurugenzi
wa Catherine Foundation, Catherine Magige akizungumza na watoto
wanaolelewa kwenye Kito cha Matumaini Village kilichopo Dodoma
alipokwenda kutoa msaada
No comments:
Post a Comment