Sunday, April 28, 2013

UNIC Dar yawahamasisha wanafunzi kujijengea utamaduni wa kusoma vitabu



Katika maadhimisho ya siku ya siku ya uandishi wa Vitabu na Hati Miliki Duniani Afisa Habari wa Kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa (katika ngazi ya Kimataifa) UNIC Bi. Stella Vuzo akizungumza na wanafunzi wa shule mbalimbali waliohudhuria semina fupi iliyoandaliwa na UNIC na kuwafafanulia umuhimu wa kusoma vitabu mbalimbali ambapo wanaweza kujifunza mambo tofauti ikiwemo kujua takwimu za ugonjwa hatari wa Malaria hapa nchini ambao umekuwa ukiongoza kwa kusababisha vifo vya watoto wenye umri chiniya miaka 5, hivyo kwa usomaji vitabu wanaweza kujua namna ya kujikinga na wanapogundua dalili kuweza kuwahi kupata matibabu.
Wanafunzi wa darasa la Saba shule ya msingi Oysterbay wakimsikiliza kwa makini Afisa Habari wa UNIC (katika ngazi ya Kimataifa) Bi. Stella Vuzo (hayupo pichani) wakati akielezea kazi zinazofanywa na Shirika la Afya Duniani WHO lililochini ya Umoja wa Mataifa katika kuhakikisha Ugonjwa wa Malaria unatokomezwa duniani katika nchini za kusini mwa Jangwa la Sahara. Ikiwa zimebaki siku mbili kuadhimisha siku ya Malaria duniani inayodhimishwa kila mwaka Aprili 25 wakati wa siku ya kuadhimisha siku ya uandishi wa vitabu na hati miliki duniani.
Msaidizi wa Maktaba ya UNIC Harriet Macha akiendesha chemsha bongo kwa wanafunzi walioshiriki semina hiyo kupima uelewa wao kuhusiana na Ugonjwa wa Malaria.
Picha juu na chini ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Usomaji na Maendeleo Bi. Demere Kitunga ambaye ni mmiliki wa Book Cafe iliyopo maeneo ya Mikocheni jijini Dar akiwaelezea wanafunzi umuhimu wa kuwa na nia na dhamira ya kujenga utamaduni wa kujisomea vitabu vya nyanja mbali mbali ikiwemo vya Kiada, Ziada na vya maarifa ambapo amewapa changamoto kujianzisha Maktaba binafsi na vikundi ambapo wanaweza kuchangishana fedha kidogo kwa uwezo wao ili kuweza kujinunulia kitabu ambacho wanaweza kushirikiana kusoma ambavyo vitawapa uwezo wa kujitambua, kuwa na maamuzi, kupata uelewa wa vitu tofauti vinavyoweza kuwajengea kujiamini na kuwawezesha kubadilisha mfumo wa maisha katika makuzi yao.
Katibu Mkuu wa Mtandao wa Vilabu vya Umoja wa mataifa Tanzania (UNCTN) Bernadetha Mshana akionyesha moja ya kitabu kilichomsaidia kuweza kupata uelewa wa kuongea Kingereza kwa urahisi zaidi ikiwa ni ushuhuda wake kwa vijana wenzake kuwa usomaji vitabu hupanua uelewa wa mtu na kujua mambo mengi.
Msaidizi wa Maktaba ya UNIC Harriet Macha (wa pili kulia) akiwa na baadhi ya walimu waliombatana na wanafunzi kutoka shule za msingi Kumbukumbu, Oysterbay na Hananasif.
Katibu Mkuu wa Mtandao wa Vilabu vya Umoja wa mataifa Tanzania Bernadetha Mshana akishirikiana uzoefu na wanafunzi wa shule za msingi za jijini Dar es Salaam wakati wa maadhimisho ya siku ya usomaji vitabu duniani na Hati miliki ambapo amesema ambapo amewataka wanafunzi hao kujiunga na vilabu vya usomaji vitabu ambavyo vitawapatia uzoefu kama ambavyo yeye vimemwezesha kujiamini kuwa na uelewa na kufikia hapo alipo sasa.
Afisa habari wa UNIC katika ngazi ya Taifa Usia Nkhoma akitoa neno la shukrani kwa wanafunzi walioshiriki semina fupi iliyoandaliwa na kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa UNIC katika maadhimisho ya siku ya uandishi wa Vitabu na Hati Miliki Duniani. Siku hii imetengwa rasmi ili kuhamasisha usomaji, auandishi na uchapishaji wa vitabu kupitia hati miliki.
Katibu Mkuu wa Mtandao wa Vilabu vya Umoja wa mataifa Tanzania Bernadetha Mshana (kushoto) akiwa na baadhi ya wafanyakazi wa Book Cafe iliyopo Mikocheni jijini Dar.
Baadhi ya wanafunzi wa shule za msingi wakisoma vitabu mbalimbali vinavyopatikana katika Maktaba ya Book Cafe yenye mandhari nzuri ya kujisomea ambapo pia panapatikana viytabu vya watu wazima vinavyohusiana na nyanja mbalimbali.

No comments: