Monday, May 27, 2013

" ANAYEDAI KUOMBWA RUSHWA YA NGONO AJITOKEZE HADHARANI."...HASHIM LUNDENGA

Hashim Lundenga.
Baada ya shutuma za rushwa ya ngono kuzidi kwa waandaaji wa shindano la Miss Tanzania, uongozi unaosimamia shindano hilo umesema kama kuna mrembo yeyote ambae amewahi kuombwa rushwa hiyo ya ngono ajitokeze.

Mkurugenzi Hashim Lundenga amesema “kuna kushutumiwa kwamba tunachukua rushwa ya ngono kutoka kwa Wasichana kitu ambacho sio kweli, hakuna msichana aliesema ameingia kambini au ameshinda kwa sababu ametoa rushwa ya ngono, katiba yetu inakataza kabisa yeyote kujihusisha na hilo”
Baadhi ya Warembo waliojitokeza 2012.
.
Toka Miss Tanzania ianze 1994 mpaka sasa kuna kesi zisizozidi nne za wazazi waliokuja kuwaondoa watoto wao kwenye kushiriki mashindano hayo baada ya kupata taarifa mbaya kuhusu hizo kashfa za ngono.

Moja ya kesi hizo ni pamoja na ya Mchungaji aliemuondoa mwanae baada ya kupewa ubalozi wa kinywaji chenye kilevi, mrembo mwingine alikua Nadya aliekua masomoni Chuo kikuu familia yake ilikataa kabisa mtoto wao kushiriki.
.
.
Lundenga amesema kuna wazazi wengine ambao walieleweshwa na wakaelewa akiwemo Mzee Muhere ambae aliposikia mtoto wake ameshinda Miss Kinondoni aliwapigia kelele sana lakini akaeleweshwa akaelewa na sasa mtoto wake anamiliki kampuni kubwa na anaendesha maisha vizuri kuliko baba yake alivyodhani.

Kwa kumalizia, Lundenga amekiri kwamba wanao utaratibu, sheria na kanuni kwenye katiba yao ambayo imepitishwa na Serikali ikiwa na maagizo mablimbali ikiwemo marufuku ya kiongozi yeyote kuomba rushwa ya ngono.
 
Pamoja na kuzushiwa hizo kashfa, amesema idadi ya Warembo wanaotaka kushiriki haijapungua bali imeongezeka kwa sababu Wasichana ndio wanazidi kujitokeza.

No comments: