BAADHI YA MATUKIO YALIYOTOKEA MTWARA MANISPAA
Baadhi ya wananchi wa
eneo la magomeni mkoani mtwara wamekimbilia katika Hospitali ya Mkoa wa
Mtwara Lugula wakihofia usalama wao kutokana na vurugu za kuchomwa kwa
nyumba zao pamoja na vibanda vya biashara zilizotokea leo asubuhi katika
eneo hilo..
Maduka maeneo ya Magomeni yamechomwa moto ikiwamo pia mali za Askari
magereza . Mwanafunzi wa CHUNO amefikishwa hospitali Ligula na majeraha ya risasi mguuni.
Mwanamke mwingine anayekadiriwa kuwa na miaka 25 mjamzito ameuawa kwa kupigwa risasi maiti ipo Ligula.
Kwa sasa( jioni hii) inaelezwa kuwa katika baadhi ya mitaa hali
imetulia na ni idadi ndogo ya wananchi ndiyo inayoonekana wakitembea
mitaani isipokua eneo la magomeni ambako mbomu yanaendelea kusikika huku
huduma za kijamii katika mji huo zikiwa zimesimama zikiwemo usafiri,
huduma za kibenki na shule
No comments:
Post a Comment