INAUMA sana! Wakati wazazi wakihenyeka na wakati mwingine kujinyima ili mabinti zao waweze kupata elimu bora itakayowasaidia maishani mwao wapo wapuuzi wanaokatisha jitihada hizo.
Mwanaume mmoja aitwaye Taliki Juma mkazi wa Temeke – Wailesi jijini Dar es Salaam ameingia katika dimbwi la AIBU baada ya kunaswa akiwa na mwanafunzi wa kidato cha pili wakifanya mchezo mchafu.
Mbaya zaidi, bila haya wala soni, Taliki alimwingiza binti huyo (jina na shule anayosoma vinahifadhiwa kwa sababu za kimaadili) katika chumba anachoishi na mwanamke anayedaiwa ni mke wake ambaye alikuwa safarini.
Chanzo chetu cha habari kilipiga simu chumba cha habari na kueleza juu ya tabia ya Taliki ya kwenda na denti huyo chumbani kwake tena akiwa kwenye sare za shule.
Kikao cha dharura kiliitishwa haraka baada ya sosi
wetu kutoa maelekezo juu ya habari hiyo ambapo kwa muda huo na foleni za
jiji la Dar usafiri uliopendekezwa ukawa ni pikipiki.
Haraka timu ya waandishi wetu ilielekea eneo la tukio lakini kwa bahati mbaya walikwama.
Taarifa
iliyopatikana kutoka kwa mtoa habari wetu ni kwamba, muda mfupi kabla
timu haijaingia eneo la tukio, Taliki alifanikiwa kukwepa mtego baada ya
kumuondoa denti huyo.
Wikiendi iliyopita Mei 18, mwaka huu chanzo chetu kilekile kilipiga tena simu kwa mwandishi yuleyule na kueleza kuwa jamaa kwa mara nyingine amemwingiza yule denti chumbani kwake.
Timu A iliondoka na kwenda moja kwa moja hadi eneo
la tukio na kuliweka chini ya uangalizi huku timu B ikielekea katika
Kituo cha Polisi cha Wailesi na kuomba ushirikiano wao.
Timu ya maaskari wa kituo hicho wakiwa tayari kwa lolote, waliungana na waandishi wetu kwenda eneo la tukio.
Binti huyo ambaye alionekana kushtuka sana baada ya kukutwa chumbani hapo, alieleza kuwa amekuwa katika uhusiano na Taliki kwa muda mrefu baada ya kumrubuni kwa fedha na zawadi mbalimbali.
Waandishi
wetu, maaskari na wazee wachache wa mtaani hapo walivamia katika chumba
hicho na kufanikiwa kumnasa laivu Taliki akiwa na denti huyo kama
walivyozaliwa akimfanyisha mambo ya kikubwa muda ambao alitakiwa kuwa
darasani.
Binti huyo ambaye alionekana kushtuka sana baada ya kukutwa chumbani hapo, alieleza kuwa amekuwa katika uhusiano na Taliki kwa muda mrefu baada ya kumrubuni kwa fedha na zawadi mbalimbali.
“Ni kweli huyu hapa ni mpenzi wangu, huwa ananipa pesa.
Nyumbani kwetu ni Mwananyamala na nimetoka nyumbani nikienda tuisheni
lakini Taliki aliniambia nije kwake.
“Naombeni mnisamehe jamani. Mama
akijua atanipiga sana. Nisameheni tafadhali na ninaahidi mbele yenu
kuwa nitaachana kabisa na huyu mbaba (Taliki),” alisema denti huyo.
Denti huyo alitoa namba ya simu ya mama yake
mzazi ambapo alipigiwa na kufika eneo la tukio na kujionea jinsi mtoto
wake anavyoharibiwa wakati yeye akiwa kwenye juhudi za kumtengenezea
maisha.
Mama wa binti huyo, hakuamini alichokiona na alijikuta akimwaga machozi muda wote, watu wazima wakapata kazi ya kumtuliza.
UPUUZI WA TALIKI
“Ni kweli nakubali huyu ni mpenzi wangu na nipo naye muda mrefu ila naombeni sana mnisamehe, kwa kweli ni shetani tu alinipitia (Mh! Huyu shetani anasingiziwa mengi sana).
“Ni kweli nakubali huyu ni mpenzi wangu na nipo naye muda mrefu ila naombeni sana mnisamehe, kwa kweli ni shetani tu alinipitia (Mh! Huyu shetani anasingiziwa mengi sana).
“Ndugu zangu
wakijua hili jambo watanitenga, naombeni muwe na roho ya huruma
(utadhani na yeye ana huruma), maisha yangu yataharibika (sijui alikuwa
anamtengenezea yule binti wa watu maisha?).”
Utetezi wake
haukusaidia na badala yake alifikishwa katika Kituo cha Polisi Wailesi
na kufunguliwa mashitaka katika Jalada namba WS/RB/585/2013 – KUFANYA
MAPENZI NA MWANAFUNZI.
credit.gumzo la jiji
No comments:
Post a Comment