Kakamega, Kenya
KUNDI la watu wenye hasira huko Kakamega lilimpiga hadi kumwua mwalimu ambaye alibambwa akifanya mapenzi na mke wa askofu.
Askofu huyo alikuwa akiendesha ibada ya mazishi kijijini Tomboo, Jimbo la Malava.
Mkuu wa Wilaya ya Kakamega Kaskazini, Gideon Ombongi , alisema mwalimu huyo na mke wa askofu walitoroka kwenye mazishi na kuingia nyumbani kwa askofu huyo ambapo ni mita chache tu kutoka mazishini.
Baada ya kukamilisha ibada ya mazishi, askofu aliingiwa wasiwasi na kuamua kumtafuta mkewe alipokwenda. Alipofika nyumbani kwake aliwakuta wawili hao wakifanya mapenzi jikoni.
Mapigano yalitokea kati ya askofu na mwalimu huyo ambapo mwanamke alikimbia.
Mkuu wa Polisi wa Kakamega Kaskazini, Justus Kitetu, alisema mapigano hayo yalivutia watu ambao walijaa kwenye nyumba ya askofu.
“Askofu aliwaambia wanakijiji kilichokuwa kimetokea nao wakampiga mwalimu na kumwua,” alisema na kuongeza kwamba askofu amekatwa kwa uchunguzi. Mke wa askofu naye alikamatwa lakini aliachiliwa.
No comments:
Post a Comment