Kuna tetesi kwamba Mwenyekiti wa Baraza la Mitihani la Taifa-NECTA ambaye pia ni Makamu Mkuuwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,Prof.Rwekaza Sympho Mukandala amegomai kubadili matokeo ya Kidato cha Nne- 2012.
Chanzo cha karibu cha Prof.Mukandala kinadai kuwa mara baada ya kutolewa taarifa ya Serikali inayotaka 'kuboreshwa' kwa matokeo hayo,Prof.Mukandala ameonesha kukataa amri hiyo hadi sasa.
"Sisi tulipitisha matokeo hayo mbele yao na kwa
idhini yao.Iweje leo Baraza libadili matokeo?.Tunafanya hivi kwa
faida ya nani na kwa ustawi wa elimu ya wapi?" alinukuliwa akihoji
Prof.Mukandala.
Habari za kuaminka zinadai kuwa Prof.Mukandala pamoja na Katibu Mtendaji Dr.Joyce Ndalichako wanajiandaa kuachia ngazi kama Serikali itasimamia uamuzi wake huo.
Habari za kuaminka zinadai kuwa Prof.Mukandala pamoja na Katibu Mtendaji Dr.Joyce Ndalichako wanajiandaa kuachia ngazi kama Serikali itasimamia uamuzi wake huo.
Hata hivyo, siku za hivi karibuni mwanahabari wetu alizungumza na
Ofisa Habari wa NECTA, John Nchimbi ambaye alisema wamekwishapokea maelekezo kwa
barua na kufanyia kazi ili kujitahidi ndani ya muda mfupi matokeo yawe
yametoka.
Nchimbi alikiri kuwapo kwa kasoro katika matumizi ya mfumo
huo mpya wa usahihishaji, kwani hawakushirikisha wadau wengi kabla ya
kuanza kutumia, lakini lengo la Baraza lilikuwa jema katika kukuza elimu
nchini
--->Ngoja tuone hatima ya vita hii ya WANASIASA na WANATAALUMA
No comments:
Post a Comment