Friday, May 24, 2013

"NILIJIUNGA CHADEMA ILI NISAIDIE HARAKATI ZA UKOMBOZI WA TANZANIA NA SINA MPANGO WA KUGOMBE UBUNGE" ... PROFESA JAY

Mchawi wa rhymes, Profesa Jay amesema hakujiunga na CHADEMA ili mwaka 2015 awanie ubunge kama wengi wanavyodhani.




Rapper huyo wa ‘Machozi, Jacho na Damu’ ambaye jina lake halisi ni Joseph Haule, ameliambia gazeti la Mwananchi la leo kuwa amejiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ili kukisaidia chama katika changamoto za kuikomboa nchi.

“Kujiunga na siasa si dhambi na haina maana kwamba nina mpango wa kugombea jimbo katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015. Sihitaji kugombea hata udiwani ila ni kwa dhumuni la kutaka kuongeza nguvu katika chama ili kuyafikia malengo,” ameliambia gazeti hilo.
 

Ameliambia kuwa yeye ni mfuasi wa Chadema tangu mwaka 2005 na amekuwa karibu na chama kwa nyakati nyingi lakini kwa sasa ameamua kuingia rasmi katika chama kama chachu katika kuongeza harakati kwa vijana.
 

“Nimeingia ili nisaidie hiki chama kuikomboa Tanzania kwani kwa muda mrefu niliokaa katika chama hiki nimegundua kuwa wamedhamiria kumkomboa msanii, kijana wa kawaida na wakubwa kwa wadogo hivyo nadhani nipo sahihi katika uamuzi wangu.”

BLA_EUCCQAEHZCc
“Natambua mimi ni mwanamuziki, sawa nina mashabiki wengi lakini haina maana kwamba sina haki ya kuchagua chama ninachoona mimi kinanifaa, lakini siwezi kusita kufanya kazi sehemu yoyote au wakati wowote chama kikinitaka nifanye kwa wakati husika,” alisema Profesa J

No comments: