Siku zote mwenye kiu iliyopitiliza
akipewa maji ya kunywa hutamani atumie jagi zaidi ya kikombe anachowekewa maji,
ndivyo ilivyomtokea mrembo Karrueche Tran aliyetoswa mwaka jana na Chris Brown
aliyemchagua Rihanna dhidi yake wakati mrembo huyo akiwa na moyo uliojaa
mapenzi na maumivu ya kulikosa penzi la ‘turn up the music singer’..
Sasa
alipopewa nafasi tena ameamua kuitumia vyema na katika kupunguza zaidi umbali
ameamua kuhamia kabisa nyumbani kwa mwimbaji huyo.
Kwa mujibu wa TMZ Chris na
Karrueche wamekua wakiishi pamoja nyumbani kwa muimbaji huyo Los Angeles tangu
walipoonekana pamoja kwenye sherehe ya kuzaliwa Chris Brown alipotimiza miaka
24.
Ripoti zinasema mrembo huyo
amehamishia nguo zake na vitu vyake takribani vyote kutoka kwake na kuvipeleka
nyumbani kwa Chris Brown lengo ni kuwa karibu zaidi na mwimbaji huyo.
Rafiki wa karibu wa KT ameuambia
mtandao wa Hollywoodlife kuwa karrueche anajaribu kuweka commitment katika
mahusiano yake na Chris ambayo mwimbaji huyo hawezi kuitunza lakini ameamua kujiweka
kwenye mstari huo kwa ajili ya mahusiano yao.
Chanzo hicho kiliongeza kuwa
Karrueche anampenda Chris kwa sababu wanaendana na anapenda upande mwema wa
Chris Brown.
Inawezekana Karrueche hamhofii tena Rihanna kwa kuwa mwaka jana alilazimika kuisomba mizigo yake kutoka kwenye nyumba ya mwimbaji huyo baada ya kumwagwa na himaya yake kuchukuliwa na RiRi bila sababu za msingi isipokuwa Chris kuamua tu kumrudisha RiRi.
Kwa sasa Chris na Rihanna hawako
pamoja tena na Karrueche anaonekana kukaba nafasi yake vizuri. Swali, je hii
pembe tatu ya mapenzi yaliyojaa drama itaishia hapo au baadae itambidi KT
aondoe tena mizigo yake kumpisha Rihanna?
No comments:
Post a Comment