Thursday, May 9, 2013

WANAFUNZI WA CHUO CHA UHASIBU WALIOKUWA WAMEFUKUZWA WAMETAKIWA KUTUMA MAOMBI UPYA


Kutokana na Chuo kufungwa, Baraza la Uongozi wa Chuo
katika kikao chake cha dharura cha tarehe 03 Mei 2013
kimeagiza wanafunzi wote kuanzia ngazi ya Cheti mpaka
Stashahada ya Uzamili kuzingatia yafuatayo:
 
1. Kila Mwanafunzi anatakiwa kutuma maombi mapya ya
kujiunga na Chuo.
2. Barua ya maombi hayo ipitishwe kwa Mkuu wa Wilaya
anapoishi mwanafunzi. Kwa mwanafunzi wa Stashahada
ya Uzamili ya Uhasibu barua yake ya maombi ipitie kwa
Mhasibu Mkuu wa Serikali.
3. Katika maombi hayo mwanafunzi anaagizwa kueleza
namna alivyoshiriki katika vurugu za tarehe 24 Aprili
2013.
4. Mwanafunzi awe amekamilisha malipo ya ada iliyobaki
wakati anatuma maombi yake.
5. Mwisho wa maombi ni tarehe 16 Mei 2013.
Maombi yapelekwe kwa anwani ifuatayo:
Mkuu wa Chuo,
Chuo cha Uhasibu Arusha
S. L. P. 2798
Arusha.
08 Mei 2013
TEMBELEA TOVUTI YA CHUO
www.iaa.ac.tz

No comments: