Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini , IGP Said Mwema akizungumza katika kikao cha Mashauriano kati ya Jeshi la Polisi na viongozi wa makanisa ya kikatoliki.kikao hicho pia kilihudhuriwa na Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki nchini Kardinali Pengo .Mkutano huo uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Mkuu
 wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Said Mwema akiwa na Askofu Mkuu wa Kanisa
 Katoliki nchini Kardinali Pengo wakiingia katika ukumbi wa mkutano 
wakati wa kikao cha Mashauriano kati ya Jeshi la Polisi na viongozi wa 
makanisa ya kikatoliki uliofanyika jijini Dar es Salaam.(Picha na Frank 
Geofray-Jeshi la Polisi) 
Na Frank Geofray-Jeshi la Polisi 
Imeelezwa
 kuwa Viongozi wa dini wana nafasi kubwa katika jamii ya kupunguza 
uhalifu kwa kuwa wao wanauwezo wa kuwabadili watu kimatendo na kifikra  
kwa kufanya doria ya mwili na roho kwa pamoja hivyo wanaweza kusaidiana 
na Polisi katika kupunguza uhalifu. 
Hayo
 yalisemwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Said Mwema wakati 
alipokuwa akizungumza katika mkutano wa mashauriano baina ya Jeshi la 
Polisi na Viongozi wa dhehebu la Romani Katoliki uliofanyika jijini Dar 
es Salaam na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali akiwemo Askofu Mkuu wa 
Jimbo kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycap Kardinali Pengo. 
Mwema
 alisema katika kipindi hiki viongozi wa dini pamoja na Jeshi la Polisi 
wanatakiwa kula njama ya kupambana na uhalifu kwa kuhakikisha kuwa 
wahalifu wote wanakamatwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria na 
Viongozi wa dini wanatakiwa watumie nafasi walizonazo katika kuhakikisha
 kuwa waumini wao wanajua mbinu za kujilinda na kuhakikisha taifa 
linakuwa salama. 
Aidha
 amewataka kutumia takwimu za uhalifiu zinazotolewa na Jeshi la Polisi 
katika kazi zao za kila siku ili kuhakikisha kuwa wale wahalifu wote 
wanaacha kutenda vitendo hivyo na wanarejea katika nyumba za ibada na 
kuwa watu wema. 
Kwa
 upande wake Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo kuu la Dar es Salaam 
Mwadhama Kardinal Pengo amesema viongozi wa dini hawawezi kukwepa jukumu
 lao la kuhakikisha kuwa uhalifu unapungua hapa nchini kwa kuwa jukumu 
hilo linaanzia kwao. 
Pengo
 alisema kuongezeka kwa uhalifu ni changamoto kwa viongozi wa dini kwa 
kuwa wao ndio wenye kazi ya kujenga maadili katika jamii na polisi 
kusimamia sheria na kuwachukulia hatua wale wanaokaidi.
Akisoma
 maazimio yaliyofikiwa katika kikao hicho Askofu Msaidizi wa Kanisa 
Katoliki Jimbo kuu la Dar Es Salaam, Mhashimu Eusebius Nzigilwa alisema 
wamekubaliana kuziimarisha kamati za ulinzi na usalama katika nyumba za 
ibada zilizopo hivi sasa wakati wakiendelea kupata mafunzo ya ukamataji 
salama kutoka Jeshi la Polisi.
“Parokia
 ambazo hazijaunda kamati za ulinzi na usalama zihakikishe zinafanya 
hivyo ndani ya mwezi huu na zile ambazo zimeundwa lakini hazifanyi kazi 
mziimarishe ili kwa pamoja tuwe salama katika nyumba zetu za 
ibada”Alisema Askofu Nzigilwa.
source:Mpekuzi huru 

 
 
No comments:
Post a Comment