Mkurugenzi
wa Shirika la Kazi Kanda ya Afrika Mashariki nchini Tanzania (ILO) Bw.
Alexio Musindo amesema kupitia msaada kutoka Serikali ya Sweden wa
kifedha ILO iliweza kuwahusisha wasichana na wavulana katika makundi
mbalimbali wenye vipato vidogo kupata uelewa wa Afya ya Uzazi kupitia
Makongamano, Semina na Mafunzo mbalimbali yaliyoendeshwa na shirika hilo
la kazi Duniani.
Ameongeza
kuwa “tuliwasaidia kuwaunganisha na vikundi vya kuweka na kukopa ili
waweze kupata mitaji midogo midogo ya kufungua biashara ndogo ndogo
katika harakati za kuwafanya wajitegemee na kuepekana na vishawishi vya
Ngono isiyokuwa Salama.
Bw.
Musindo amesisitiza Umuhimu wa TACAIDS kuandaa makongamano kama haya
ili kuwawezesha wasichana na wavulana wadogo kupata ufahamu uelewa na
mafunzo ya uzazi wa Afya na jinsi ya kuelewa mabadiliko yao ya
kimaumbile.
“Ni
matumaini yangu mwingiliano huu wa Utamaduni wa kupambana na Ukimwi,
Kinga na Uwezeshwaji wa Kiuchumi umefanyika vizuri, hasa katika
kuyalenga makundi yaliyo katika mazingira magumu itasaidia kuongeza kasi
ya kupunguza maambukizi mapya kama ilivyoripotiwa na ripoti ya UNAIDS
mwaka 2012 Duniani kwamba maambukizi mapya yamepungua kwa Asilimia 20”.
Amesema.
Sehemu ya washiriki wakifuatilia mada mbalimbali zilizowasilishwa leo kwenye Kongamano hilo.
Mgeni
rasmi Katibu Mkuu wa Wizara ya Jamii, Jinsia na Watoto Bi. Kijakazi
Mtengwa akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Wizara hiyo amesema mikakati
ya kuwawezesha Wanawake Kiuchumi inaweza kupunguza hatari ya kupata
maambukizi ya Virusi vya Ukimwi kwa Wanawake, Wasichana na Wavulana
wadogo.
Amesema
Jamii lazima itambue kuwa juhudi zaidi zinahitajika ili nchini yetu
iweze kufikia malengo ya 0.3 yaani Tanzania ambayo haina maambukizi
mapya ya VVU, Ukimwi usiwe sababu ya vifo, vile vile pasipo unyanyapaa
wala ukatili kwa mtu yeyote anayeishi na Virusi vya Ukimwi.
Mwenyekiti
wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) Dr. Fatma Mrisho akizungumza na
washiriki amesema Takwimu zinazonyesha Wanawake wako katika hali ya
hatari ya kuambukizwa zaidi kuliko wanaume ambapo mpaka sasa ni Asilimia
Sita ya Wanawake nchini huambukizwa wakati wanaume ni Asilimia 3 nchini
nzima.
Dr.
Mrisho alisisitiza umuhimu wa kumwezesha mwanamke kiuchumi kama ndio
moja ya suluhisho la kumfanya kutokuwa tegemezi katika jamii.
“Amesema
takwimu zinazonyesha katika nchi nyingi za Kiafrika umaskini unachagia
sana kuenea kwa Ukimwi maana Wanaume wengi hutumia umasikini wa
Wasichana au Kinadada kuwarubini kwa fedha na kufanya nao Ngono
isiyosalama”.
Dr.
Fatma Mrisho amepongeza juhudi za ILO na kuwataka mashirika mengine na
wadau wa mapambano dhidi ya Ukimwi kuiga juhudi zilizofanywa na ILO za
kuandaa makongamano ya kiuchumi ili kumwezesha Mwanamke na wavulana
wadogo kujitambua na kuelewa jukumu lao katika mapambo ya VVU na Ukimwi
nchini.
Meza
Kuu: Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la
Ukimwi Tanzania (UNAIDS) Dr. Hedia Belhadj, Mwakilishi kutoka TUCTA Bw.
Hezron Kaaya, Katibu Mkuu wa Wizara ya Jamii, Jinsia na Watoto Bi.
Kijakazi Mtengwa, Mwenyekiti wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) Dr.
Fatma Mrisho, Mkurugenzi wa Shirika la Kazi Kanda ya Afrika Mashariki
nchini Tanzania (ILO) Bw. Alexio Musindo, Mkurugenzi wa Sera na Utetezi
wa Chama cha waajiri Tanzania (ATE) Bi. Justina Lyela.
Mwakilishi
kutoka shirikisho la wafanyakazi Tanzania (TUCTA) Bw. Hezron Kaaya
alisisitiza mshikamano na umoja wa wafanyakazi katika mapambano ya VVU
na Ukimwi sehemu za kazi.
Bw.
Kaaya amesisitiza majadiliano kama hayo yasiishie kwenye makabrasha
bali wayatekeleze kwa vitendo ili kuleta matokeo chanya kwenye jamii.
Mkurugenzi
wa Sera na Utetezi wa Chama cha waajiri Tanzania (ATE) Bi. Justina
Lyela akitoa nasaha zake kuhusu viwango sawa vya malipo ya mishahara kwa
wafanyakazi nchini ili kuwakomboa wanawake na kipato kidogo makazini.
Picha
juu na chini ni sehemu ya washiriki kutoka ndani na nje ya nchini wa
Kongamano la kuwawezesha Kiuchumi Wanawake, Wasichana na Wavulana dhidi
ya Maambukizi ya Virusi vya Ukimwi lililofanyika leo jijini Dar na
kuratibiwa kwa pamoja kati ya ILO na TACAIDS.
Washiriki wa Kongamano hilo wakiangalia baadhi ya machapisho mbalimbali ya VVU na Ukimwi.
Picha
juu na chini mgeni rasmi katika picha ya pamoja na washiriki wa
Kongamano hilo la siku moja lililofanyika jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment