POLISI wa kike wa Kituo cha Magomeni, jijini Dar es Salaam aliyejulikana kwa jina moja la Anisa, ametimuliwa kazi kwa madai ya kupiga picha ya utupu iliyosambaa mitandaoni.
Chanzo
makini ndani ya jeshi hilo kilisema Anisa alifukuzwa kazi wiki
iliyopita baada ya kuhojiwa na mabosi wake wa makao makuu ya jeshi hilo
na kukiri kuwa picha hiyo ni yake.
“Anisa
aliitwa makao makuu, mabosi wakamuonesha picha yake akiwa mtupu
kitandani, akakiri ni yeye. Alijitetea eti alifanya hivyo kwa sababu
siku ya tukio alikuwa amelewa sana,” kilisema chanzo.
Chanzo
kiliendelea kudai kwamba baada ya afande huyo mwenyeji wa Tanga kukiri,
viongozi wa jeshi hilo walimwambia amekiuka kanuni na kulidhalilisha
jeshi hilo hivyo hataendelea kuwa mtumishi.
Picha ya afande huyo imeenea
mitandaoni na kwenye baadhi ya simu za mikononi za watu kitendo
kulicholifanya jeshi hilo kufanya uchunguzi na kubaini kuwa ni yake.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina, Suleiman
Kova alipoulizwa juzi alikiri kufukuzwa kwa askari huyo na kumtaka
mwandishi wetu kufuatilia zaidi kwa Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi
Kinondoni, ACP Camilius Wambura ambaye naye alipoulizwa kuhusu tukio
hilo alikiri.
‘‘Tunahitaji askari wenye
maadili mema ndani ya jeshi letu, yule atakayefanya mambo bila kufuata
kanuni na sheria hatua kali zitachukuliwa dhidi yake. Askari muda wote
anatakiwa awe mfano bora kwa jamii,’’ alisema Afande Wambura.
Taarifa zaidi zinadai kwamba kwa sasa Anisa anaishi uraiani kama raia wa kawaida
source:Mpekuzi huru
No comments:
Post a Comment