Monday, June 3, 2013

RASIMU YA KATIBA MPYA YAPENDEKEZA KUWEPO KWA SERIKALI TATU.....


Leo ni ufunguzi wa rasimu  ya katiba  mpya  na Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba amesema  kwamba  Rasimu hiyo  imependekeza kwamba matokeo ya rais yahojiwe mahakamani.

Kwa lugha nyingine ni kwamba katiba ijayo itaruhusu Rais kushtakiwa mahakamani endapo matokeo yake yatatiliwa shaka na wagombea wengine. 
Jaji Warioba ameyasema hayo  wakati wa uzinduzi wa Rasimu ya Katiba Mpya katika tukio la kihistoria nchini Tanzania.

"Imependekezwa kwamba matokeo ya Rais yatashikiwa mahakamani lakini kwa masharti," amesema Jaji Warioba hivi punde.

Jaji Warioba ametaja masharti hayo ni kwamba wagombea wa urais ndio watakuwa na haki ya kuhoji matokeo ya rais na si vinginevyo. Pili, matokeo hayo yanatakiwa kuhojiwa ndani ya mwezi mmoja tu na si vinginevyo.

Amesema pia tume imependekeza kuwapo kwa wabunge wa aina mbili ambao ni wabunge wa kuchaguliwa na wabunge wengine wa kuteuliwa na Rais.
 Pia amesema kwamba kutakuwapo kwa utaratibu wa wanawake kugombea katika majimbo. Kwa maana hiyo hakutakuwapo  wabunge wa Viti Maalumu.
Pamoja  na hayo, tume ya jaji Warioba imependekeza   kuwepo  kwa  serikali tatu ambazo ni  -serkali ya zanzibar, ya tanganyika na ya muungano.
mambo ya muungano  yaliyopendekezwa:
1)katiba ya jamhuri ya muugano wa tanzaia
2)sarafu na benki kuu
3)mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa
4)ushuru
5)ulinzi na usalama
6)usajili wa vyama vya siasa
7)uraia na uhamiaji

No comments: