Hatua hiyo imekuja baada ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba Mpya kutangaza rasimu iliyotoa mwelekeo wa kupatikana kwa Katiba Mpya ya Tanzania.
Akizungumza jana na gazeti la Mwananchi, Katibu Mkuu wa Chama cha NCCR-Mageuzi, Samweli Ruhuza amesema hali hiyo inaweza kuleta changamoto kubwa hivyo muda sahihi wa vyama vichanga kuzungumzia hili ni sasa.
Katibu mkuu wa chama cha Kijamii (CCK), Renatus Muhabi anaunga mkono hatua ya kuunganisha vyama hivyo kwa lengo la kuwakilisha mawazo yao kwa maslahi ya taifa
No comments:
Post a Comment