Thursday, June 27, 2013

WANAWAKE MSIENDE KWA KARUMANZILA, UKWELI NI HUU HAPA...!



Stacey Tantleff-Dunn mtalamu wa afya ya ulaji na mwonekano anasema kwamba, vipimo vya uzuri kwa wanawake vimegawanyika. Kwa kawaida wanaume hupima uzuri wa mwanamke kwa sura au mwili, lakini linapokuja suala la kupata mtu ambaye wanataka kuishi naye kama mke, suala la haiba, yaani tabia na mwenendo, linachukua nafasi kubwa.

Wale wanawake ambao wanapendeka, ambao wana haiba na mienendo mizuri hata kama wangekuwa wabaya kwa sura na umbo, bado wako kwenye nafasi ya kuhesabiwa kuwa ni wazuri. Hawa ndiyo ambao hupata wanaume kirahisi. Wataalamu wa uzuri, hivi sasa wanasisitiza kwamba, kama mwanamke anataka kweli kuingia mahali ambapo ataanza kuonekana ni mzuri katika maisha yake yote, inabidi ajifunze kuwa na haiba na mwenendo unaovutia.

Uzuri wa sura na umbile huwavuta wanaume kuwa karibu na mwanamke na kuanzisha uhusiano, hasa wa kimwili. Lakini, hivi sasa imebainika kwamba, haiba na mwenendo wa mwanamke ndizo silaha zake, linapokuja suala la mwanaume kufanya uamuzi wa aishi na nani. Pamoja na kujali sura na umbo, haiba bado ndiyo kigezo cha ndani kabisa cha uamuzi. 

“Inaonekana wanaume wanarejea kwenye mfumo wa kale kabisa wa kuoa kufuatana na uwezo wa mwanamke kufanya kazi za kuzalisha, kutunza watoto na familia, kwa kuangalia familia alimotoka. Hii ina maana kwamba, uzuri wa sura na umbo kwa wanawake unabakia zaidi kwenye biashara.”

Tafiti zinaonyesha kwamba, hivi sasa wanaume wameanza pia kujali zaidi uzuri wa kutenda. Wanaume wengi wanaangalia kama mwanamke anaweza kuifanya familia kuwa imara kimapato na kimaadili, kuliko kufikiria uzuri na usomi. Inaonekana wanaume wanarejea kwenye mfumo wa kale kabisa wa kuoa kufuatana na uwezo wa mwanamke kufanya kazi za kuzalisha, kutunza watoto na familia, kwa kuangalia familia alimotoka. Hii ina maana kwamba, uzuri wa sura na umbo kwa wanawake unabakia zaidi kwenye biashara.

Ni wazi wanawake wazuri kwa sura na umbo, wana soko la haraka kwa wanaume. Hivyo ni wanawake wa kuchezewa zaidi kuliko kuolewa. Hata ukiacha tabia, wanaume wamefundishwa kuogopa wanawake wazuri sana. Wanaamini kwamba, mwanamke mzuri sana anaweza kusumbua sana. Na ni kweli, wengi husumbua, hasa wakishajua kwamba, wana uzuri wa kiwango kikubwa.

Watafiti wanakiri kwamba, wanawake wazuri sana kwa sura na umbo, huwa wanawasababishia waume zao maradhi ya moyo, shinikizo la juu la damu, kuharibu shughuli zao na hata kuwafanya kupata matatizo fulani ya kiakili. Hii inatokana na wanaume hao kuwa katika mashaka ya wake zao kuchukuliwa muda wowote kutokana na uzuri wao.

Ndiyo maana takwimu zinaonyesha kwamba, wanaoolewa zaidi hivi sasa ni wale wanawake ambao jamii imekuwa ikiamini kuwa ndiyo wabaya kwa sura au umbo, lakini ambao wana haiba na mienendo mizuri. Hata ndoa zinazodumu, inaelezwa kwamba, ni zile za wanawake wabaya kwa sura au umbo lakini ambao wana haiba na mienendo mizuri. Ndoa za wanawake wazuri kwa sura na umbo, hazina umri mkubwa…….

No comments: