Majina ya askari saba wa Tanzania waliokufa kwenye shambulio la ghafla mjini Darfur yamepatikana.
Askari
hao waliokufa ambao walikuwa kwenye vikosi vya kulinda amani vya Umoja
wa Mataifa huko nchini Sudan ni Sajenti Shaibu Othuman, Koplo Oswald
Chaula, Koplo Mohamed Juma, Koplo Mohamed Chikilizo, Pte. Rodney
Ndunguru, Pte. Peter Werema na Pte. Fortunatus Msofe.
Kwa
mujibu wa taarifa zilizopatikana kwenye mtandao ni kwamba askari hao
walikwenda kujaribu kumwokoa mwenzao (ambaye hakutajwa) ambaye
alisemekana kutekwa na vikosi vya waasi nchini humo.
Wakati wakijiandaa, ghafla walizingirwa na askari hao waasi na kisha kushambuliwa kwa risasi hadi kufa.
Haikufahamika hali ya askari huyo ambaye alidaiwa kutekwa kama bado yu hai ama ni miongoni mwa waliokufa.
Mungu azilaze roho za askari wetu mahali pema peponi, Amina
MPEKUZI
No comments:
Post a Comment