Friday, July 19, 2013

WALIOJIFANYA MASISTA WA KIKATOLIKI WAKAMATWA UWANJA WA NDEGE WAKISAFIRISHA MADAWA YA KULEVYA..!!

Wasafirishaji hao walisimamishwa wakati wakiwasili kwenye kituo maarufu cha mapumziko nchini Colombia, sababu polisi walifikiri kwamba mavazi yao hayakuwa yakionekana halisia.

Maofisa waligundua kwamba kila mwanamke kati yao alikuwa na zaidi ya kilo 4 za cocaine zikiwa zimefungwa katika miguu yake.
Wakiwaongezea fedheha katika mashitaka, wasafirishaji hao walipangwa mstari mbele ya waandishi wakiwa bado wamevalia mavazi yao ya kituko kuficha ukweli.
Wanawake hao watatu, wenye umri wa miaka 20, 32 na 37, walitua kwa ndege kwenye kisiwa hicho cha San Andres kutoka Bogota siku ya Jumamosi asubuhi.
Kapteni wa Polisi Oscar Davila alisema wanawake hao walionekana kama wamechanganyikiwa, na kuongeza kwamba mfumo wa tabia zao haukuonekana kuwa sahihi.
Pale masista hao bandia waliposimamishwa na kupekuliwa, walikutwa wakiwa na shehena kubwa ya cocaine ikiwa imefungwa katika miili yao.
Wote watatu waliangua kilio na kusisitiza kwamba walitumiwa tu kusafirisha dawa hizo sababu ya matatizo yao ya kifedha, alisema Davila.
Wanawake hao walikamatwa na kuswekwa rumande kwa mashitaka ya kusafirisha dawa za kulevya.
Dawa hizo zilikadiriwa kuwa na thamani ya Dola za Marekani 35,000 mtaani, kwa mujibu wa Kamishna wa Polisi wa mji huo, Jorge Gomez.
"Hawakuwa wafuasi halisi wa dini, hawakuwa masista," alisema. "Kinyume cha hilo, walikuwa wakitumia mwanya huo kwa ajili ya kazi hii.
"
San Andres, iliyoko Caribbean nje ya ufukwe wa Nicaragua, ni moja ya mahali maarufu kabisa nchini Colombia kwa ajili ya wakazi na watalii.
Hatahivyo, inatumika pia kama njia kuu ya kupitishia dawa za kulevya kwa ajili ya kusafirisha cocaine kati ya Colombia bara na Amerika ya Kati
Wanawake watatu wamekamatwa kwa madai ya kujaribu kusafirisha dawa za kulevya kupitia uwanja wa ndege wakiwa wamevalia kama masista.

No comments: