Kupitia
taasisi yake ya kutoa misaada, nahodha wa Ivory Coast na gwiji wa
Chelsea Didier Drogba atasaidia ujenzi wa kliniki tano za watoto na
wanawake katika nchi yake. Tangazo hilo lilitolewa na katibu mkuu wa
Didier Drogba Foundation Guy Roland Tanoh, ambaye alisema kwamba ujenzi
wa kliniki hizo utafadhiliwa na Taasisi ya London galas pamoja na fedha
Drogba mwenyewe.
Kutoka SuperSport:
Tanoh amesema kiasi cha 2.5 billion CFA francs ($5 million) kitatumika kuwekeza katika ujenzi wa kliniki hizo, huku zikijengwa katika miji mitano mikubwa ya nchi hiyo Abidjan, Yamoussoukro, Man, Korhogo na San Pedro.“Drogba aliendesha mchango huko London na zikapatikana kiasi cha $ 2 billion CFA francs ($4 million),” Tanoh alisema. “Kiasi kilichobakia cha million francs ($1 million) hakitakuwa tatizo kuona ndoto ya mwenyewe Drogba ya kuona afya za wananchi wa Ivory Coast zinapewa kipaumbele.”
Drogba mara ya kwanza alitangaza mpango wake wa kujenga hospitali kubwa katika jiji la Abidjan mwaka 2009 akitumia fedha zote - kiasi cha £3 million ($4.5 million) alicholipwa
na Pepsi. Lakini badala ya kujenga hosptali hiyo moja kubwa akaamua
ambayo ingekuwa mjini tu, akaamua kujenga vituo vitano vya afya katika
mikoa mingine ili kuweza kusambaza vizuri huduma za afya.
No comments:
Post a Comment