Msanii mahiri wa Kughani Mashairi
kwa mtindo wa kisasa kabisa,Mrisho mpoto akizungumza mbele ya sehemu ya
wakazi wa Mkoa wa Dodoma na vitongoji vyake waliojitokeza mapema leo
asubuhi kwenye semina ya kamata Fursa twendzetu,iliofanyika ndani ya
moja ya ukumbi wa hotel ya Africans dream,iliyoko nje kidogo ya mji wa
Dodoma. Semina
ya Kamata Fursa twendzetu inayoratibiwa na Clouds Media
Group,imekwishafanyika mikoa zaidi ya mitano ikiwemo
Kigoma,Tabora,Singida,Mtwara, Mbeya,Iringa sambamba na leo ndani ya
Dodoma,ambo semina hizo zote zimeonesha mafanikio makubwa kwa vijana
kwali walikuwa wakijitokeza kwa wingi kwenye ushiriki.
Sehemu ya washiriki wa semina hiyo ilipokuwa ikiendelea mapema leo asubuhi.
Wakifuatilia kwa makini mada
mbalimbali zilizokuwa zikitolewa kwenye semina hiyo ya kamata fursa
twendzetu,mapema leo asubuhi mkoani Dodoma.
Mwakilishi wa NSSF-Makao
Makuu,Salim Khalfan akifafanua masuala mbalimbali yatokanayo na faida za
kujiunga na shirika hilo la NSS,ndani ya semina ya kamata fursa
twendzetu iliofanyika mapema leo kwenye moja ya ukumbi wa hotel ya
Africans dream,iliyoko nje kidogo ya mji wa Dodoma.
Sehemu ya ya watu wakifuatilia kwa umakini yaliyokuwa yakijiri kwenye semina hiyo.
Meneja wa NSSF mkoani
Dodoma,Bwa.Kirondera Nyabuyenze akizungumza fursa mbalimbali zitokanazo
na shirika la NSSF,Nyabuyenze amewataka watu mbalimbali wajitokeze kwa
wingi kujiunga na NSSF,ili kujipatia fursa mbalimbali zikiwemo
mikopo,matibabu na mambo mengiyo mbalimbali.
Mwakilishi wa Kampuni ya
Maxmalipo,Renard Munuri akizungumza kwenye semina ya Kamata Fursa
Twenzetu kwa vijana,kuhusiana na masuala mbalimbali yanayofanywa na
kampuni yake katika kusaidia huduma za jamii,ndani ya moja ya ukumbi wa
hotel ya Africans dream,iliyoko nje kidogo ya mji wa Dodoma.
Mmoja wa Watangazaji mahiri wa
Clouds FM,akizungumzia fursa mbalimbali alizokumbana nazo na namna
alivyozifanyia kati na kujipatia sehemu ya mafanikio katika kupambana
na maisha.Semina ya Kamata Fursa twendzetu inayoratibiwa na Clouds Media
Group,imekwishafanyika mikoa zaidi ya mitano ikiwemo
Kigoma,Tabora,Singida,Mtwara, Mbeya,Iringa sambamba na leo ndani ya
Dodoma,ambo semina hizo zote zimeonesha mafanikio makubwa kwa vijana
kwali walikuwa wakijitokeza kwa wingi kwenye ushiriki.
Baadhi ya wasanii ambao
wamenufaika mara baada ya kujiunga na Shirika la NSSF,shoto ni Queen
Doreen na Mwasiti wakijadiliana jambo na mdau Phillipon mapema
leo,wakati semina ya Kamata fursa twendzetu ilipokuwa ikiendelea.
Sehemu ya wakazi wa mji wa Dodoma wakiwa wamejitokeza mapema leo asubuhi kwenye semina ya fursa kwa vijana
Sehemu ya meza kuu ya watoaji mada wakishangilia jambo.
PICHA ZAIDI BOFYA MICHUZIJR.BLOGSPOT.COM.
No comments:
Post a Comment