Pichani ni Waziri wa Mambo ya Ndani, DR. William Nchimbi, akimpa pole Balozi Isaac Sepetu alipomtembelea kumjulia hali nyumbani kwake September 21, 2013.
Balozi Abraham Isaac Sepetu amefariki dunia mapema leo akiwa katika hospitali ya TMJ alikokuwa amelazwa akitibiwa ugonjwa wa Kisukari na kiharusi alioupata hivi karibuni mjini Zanzibar. Balozi Sepetu, ambaye pia ni baba mzazi wa Miss Tanzania 2006, Wema Isaac Sepetu, hadi anapatwa na ugonjwa na hatimaye mauti, alikuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Uwekezaji wa Vitega Uchumi Zanzibar. PICHA: Maktaba/GPL
No comments:
Post a Comment