Labda
kwa wale wasiofahamu niwaambie tu kwamba dhana ya mapenzi ni dhana
yenye wigo mpana sana na ndiyo maana hutasikia hata siku moja
tumepumzika kuizungumzia.
Hata hivyo, tunachofanya siku zote ni kukumbushana kwa yale
tunayoyafahamu na kushauriana kwa pale tunapohisi wengi hufanya makosa.
Baada ya kusema hayo sasa nigeukie mada yangu ya leo ambayo kwa kiasi
kikubwa inawahusu wale walio kwenye ndoa na kikubwa nazungumzia yale
ambayo wawili waliotokea kupendana kwa dhati wanatakiwa kuyafanya mara
baada ya kumaliza kufanya tendo la ndoa.
Nalazimika kuandika makala haya baada ya kubaini kuwa wengi wamekuwa
wakifanya makosa na kujikuta wakishamaliza kufanya tendo hilo takatifu,
kila mmoja anageukie kwake kisha kuuchapa usingizi.
Sisemi kwamba ni
lazima kuyafanya haya nitakayoyaeleza leo ila yakifanywa huwa na
manufaa yake na mara nyingi yanaboresha uhusiano.
Kuoga pamoja
Mtakuwa ni watu wa ajabu kama
mtamaliza kufanya tendo hilo kisha kila mmoja kulala na majasho yake.
Wapo wasiojali katika hili na kuona kuoga au kutooga ni uamuzi wa mtu.
Elewa linapokuja suala la usafi inashauriwa mkimaliza lazima muoge.
Wapo wanawake ambao wakishamaliza hukimbilia kuwaandalia maji wenza
wao, wakishaoga ndipo nawo huenda kuoga. Hivi unaona ugumu gani kwenda
kuoga na mwenza wako? Unaijua raha ya kuoga na huyo wako wa maisha?
Wanaofanya hivyo wanajua raha yake na wewe ambaye hujawahi, anza leo.
Mmemaliza mambo yenu, chukuaneni kimahaba, elekeeni bafuni kisha
ogeshaneni kimahaba.
Baada ya hapo rudini chumbani, mkishajifuta maji pandeni kitandani mkiwa wapesi.
Kusifiana
Hakuna muda maalum uliotengwa kwa
ajili ya wanandoa kusifiana. Hilo linaweza kufanyika wakati wowote
lakini pale mnapomaliza kufanya tendo la ndoa ni lazima utakuwa na jambo
zuri la kumuambia mwenza wako.
Msifie kwa utundu na ubunifu wake.
Msifie pia kwa mapenzi matamu anayokupa na ikibidi mpe sifa ya uzuri
wake kiasi cha kukufanya kila unapokuwa karibu yake ujisikie amani ya
kupitiliza.
Wapo ambao hawana kabisa kasumba ya kuwasifia wala kuwashukuru wenza
wao kwa mazuri wanayofanyiwa. Yaani wao wanachukulia kila kitu poa tu
bila kujali kwamba kusifiana kunanogesha mambo.
Kuelekezana
Kwenye kale kamchezo, wapo ambao
wanakosea, kuelekezana na kukosoana kwa wapenzi ni jambo la kawaida.
Yawezekana mwenza wako alifanya kitu ambacho hakikukufurahisha wakati
mkiendelea na burudani yenu, mnapomaliza mwambie lakini kwa lugha ya
kimahaba na ya upole. Naamini kwa kufanya hivyo atakuelewa na
kubadilika.
Zungumzieni maisha
Huu ni wakati muafaka wa
kujadili changamoto na malengo katika maisha yenu. Hapa akili zinakuwa
zimetulia na kila mmoja anakuwa na mawazo chanya kwa mwenza wake.
Jadilini mambo yenu, wekeni mikakati ya kuliboresha penzi na maisha yenu
kwa ujumla.
Hayo ni baadhi ya mambo ambayo mnashauriwa kuyafanya pale
mnapomaliza kufanya tendo la ndoa.
Yapo mnayotakiwa kuyaepuka ili
kutotibua furaha iliyopatikana. Hayo nitakuja kuyaeleza katika makala
zinazokuja kupitia ukurasa huu. |
No comments:
Post a Comment