Mtoto
wa kiume aliyepata utambulisho wa nguo aliyokuwa amevaa ‘the boy in
yellow’ alijikuta anachukua ‘attention’ ya waumini wote waliohudhuria
siku ya familia St Peter’s Square huko Vatican baada ya kuvamia jukwaani
na kukaa na papa Francis kwa muda wa dakika kadhaa.
Kiongozi
mkuu wa kanisa Katoliki Papa Francis alikuwa akizungumza mbele ya umati
mkubwa wa familia mbalimbali zilizohudhuria sherehe za siku ya familia.
Baada ya mtoto huyo kupanda jukwaani alienda mbele ya papa na kumtazama
na kuzunguka hapa na pale japo hakufanya fujo ya aina yoyote.
Makadinali
walijaribu kutumia njia za kumshawishi kutoka kama kumpatia pipi,
lakini mtoto huyo aligoma kuondoka. Papa alimgusa kichwani na kutabasam
akamwacha na kuendelea na alichokuwa akikifanya.
Kuna wakati papa akiwa amesimama anazungumza mtoto huyo alimkumbatia miguu lakini papa alimwacha.
Baadaye
Vatican walishare moja ya picha za tukio hilo katika akaunti yao ya
Instagram ikimwonesha mtoto huyo akiwa amekalia kiti cha papa na
kuandika ‘A special guest with #popefrancis.
Source: Mail Online
No comments:
Post a Comment