Sunday, February 3, 2013

Maumivu wakati wa hedhi(Dysmenorrhoea)

Written By Nicolaus Trac on Monday, January 28, 2013 | 7:32 AM

Clinic Yetu na Dr.Paul Masua
Wanawake wengi hupata maumivu wakati wa hedhi.  Mara nyingi maumivu  si makali,lakini mwanamke 1 katika ya wanawake 10 hupata maumivu  makali ya kutosha  kuathiri shughuli za kila siku. Maumivu yanaweza kuwa makali kiasi kwamba wanashindwa kwenda shule au kufanya kazi. Madaktari wanaita maumivu wakati wa hedhi dysmenorrhoea.

Maumivu haya yamegawanya katika makundi mawili
-Primary dysmenorrhoea-haya ni maumivu yanayotokea bila sababu ya msingi.Mara nyingi sababu haijulikani. Mara nyingi hutokea katika vijana na wanawake katika umri wa miaka 20.
-Secondary dysmenorrhoea- haya ni maumivu yanayosababishwa na matatizo kwenye mfuko wa uzazi au kwenye nyonga.Hutokea mara nyingi kwa wanawake kati ya miaka 30-40.

Dalili za primary dysmenorrhoea
Zifuatazo zinaweza kuwa dalili za tatizo hili

-Maumivu yanaweza kusambaa kuelekea kwenye mgongo na miguu
-Kwa kawaida huanza pale mwanamke anapoingia kwenye siku zake ingawaje huweza kuanza kabla ya kuingia kwenye siku.
-maumivu hudumu kwa muda wa saa12-24 hata hivyo yanaweza kuendelea kwa muda wa siku 2-3
-yanaweza kubadilika kila mzunguko.
- hupungua ukali mwanamke anapokuwa au kupata mtoto.

Kwa wagonjwa wengi daktari anaweza kutambua tatizo baada ya kuuliza maswali. Pia anaweza kupima tumbo. Mara nyingi hakuna vipimo vyovyote vinavyojitajika.

Dalili za secondary dyamenorrhoea
Mara nyingi tatizo hili husababisha na magonjwa mfano maambukizi kwenye kizazi(PID),endometriosis,uvimbe kwenye mfuko wa uzazi nk

Dalili za tatizo hili ni maumivu wakati wa hedhi, na dalili nyingine ni 
-kubadilika kwa mzunguko
-kuvuja damu katikati ya hedhi.
-maumivu wakati wa kujamiina.
-maumivu katikati ya mzunguko.
-kuvuja damu nyingi.

Daktari anaweza kupima tumbo na njia ya kizazi kisha anaweza kuagiza ultrasound au vipimo vingine
Matibabu
Primary dysmenorrhoea
Dawa za maumivu zinatumika kutibu vizuri tatizo hili.
Pia njia za uzazi wa mpango zinaweza kutumika kutibu tatizo hili.

Secondary dysmenorrhoea 
Matibabu hutegemea tatizo. Hivyo antibiotiki zinaweza kutimika kama kuna maambukizi kwenye kizazi.

No comments: