Silaha
zaina hii na nyingineza zikiwamo ndogo na nyepesi zimekuwa
zikisababisha madhara makubwa kwa maisha ya watu wasio na hatia pamoja
na ubaribifu wa mali zao. takwimu zinaonyesha kwamba watu zaidi ya nusu
milioni hufa kila mwaka ikiwa ni pamoja na wanawake 66,000 na wasichana
kutokana na matumizi mabaya ya silaha. Aidha kwa mujibu wa Ofisi ya
Umoja wa Mataifa inayoshughulikia masuala ya silaha, takwimu zinaonyesha
kwamba kati ya mwaka 2000 na 2010, karibu wafanyakazi 800 wa misaada
waliuawa katika mashambulizi huku wengine 689 walijeruhiwa
Na Mwandishi Maalum
Macho
na Masikio ya Dunia yameelekezwa hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa (
UM) ambako zaidi wa wajumbe 2000 kutoka mataifa 193 wanakutana katika
kile kinachoitwa mkutano wa mwisho kuhusu Mkataba wa Kimataifa wa
kudhibiti Biashara ya Silaha ( ATT).
Mkutano
huu umeanza siku ya jumatatu kwa kufunguliwa na Katibu Mkuu Ban Ki
Moon. Akiwazungumza wajumbe hao, Mkuu huyo wa UM, pamoja na mambo
mengine ameeleza kwamba kama jumuiya ya kimataifa imeweza kuweka viwango
vya kimataifa vinavyodhibiti utengenezaji wa T-shirt, midoli na
uzalishaji na uuzaji wa nyanya kwanini ishindikane kudhibiti na kuweka
viwango kwenye silaha.
Akasema
Ban Ki Moon “ Tumeweka viwako karibu katika kila bidhaa kuanzia
utengenezaji wa T-shirt, midoli hadi kwenye nyanya, lakini si biashara
ya silaha” akahoji Ban Ki Moon
Na kwa
sababu hiyo amewataka washiriki wa mkutano huu kuonyesha dhamira ya
kisiasa ya kukamilisha majadiliano ili hatimaye ifikapo Marchi 28 ambayo
ndiyo siku ya mwisho ya mkutano watoke na Mkataba, kama ilivyoainishwa
kwenye mkutano wa tisa kwamba mkutano huu ni wa mwisho.
Akaenda
mbali zaidi kwa kuwahadharisha wajumbe kwamba wanapokutana katika
mkutano huu, hawaanzi upya majadiliano ya mkataba, majadiliano ambayo
yalifanyika tangu mwaka 2006 wakati mchako wa ATT ulipoanza. Bali
wanakuta kukamilisha kazi ya kutoka na Mkataba.
Mkutano
huu unafanyika ikiwa ni mwaka mmoja tangu kumalizika kwa mkutano wa
Kihistoria uliofanyika mwaka jana ( 2012) ambapo kulikuwa na matumaini
makubwa kwamba mkutano ule ungemalizika kwa kutoka na Mkataba lakini
hali haikuwa hivyo.
Ujumbe
wa Tanzanzia katika mkutano huu muhimu unaongozwa na Balozi Ramadhan
Mwinyi, Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Ubalozi wa Tanzania katika Umoja
wa Mataifa.
Ujumbe
huu unawahusisha wataalam kutoka Vyombo vya Ulinzi na Usalama, Wizara
ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu,
TRA na wajumbe wawili kutoka Asasi isiyo ya kiserikali.
Kwa
ujumla ujumbe wa Tanzania umejipanga vema katika kufuatilia kila hatua
ya majadiliano, kutoa msimamo wa Tanzania na kuhakikisha kwamba maslahi
ya nchi yanalindwa.
Akichangia
majadiliano ya jumla, Balozi Mwinyi alieleza bayana kwamba, nia ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni kwamba Mkataba huo unalenga wanachama
wote.
Aidha
akafafanua zaidi kwa kusema Tanzania inaamini kwamba lengo na madhumuni
ya Mkataba huo ni kudhibiti biashara haramu ya silaha bila ya kuathiri
haki ya mataifa kujilinda kama ilivyoainishwa kwenye Katiba ya Umoja wa
Mataifa.
Vilevile
akaeleza kwamba Mkataba huo hautaingilia haki ya mataifa kuishi kwa
amani na usalama, kufurahia uhuru wao na kujiletea maendeleo, lakini
kubwa zaidi ni kwamba mkataba huo haulengi kupokonya silaha bali
kudhibiti.
Baadhi
ya wazungumzaji hususani wale wanaotoka nchi kubwa wameanza kuweka
mikingamo yao kwa kutoa kauli za kutahadharisha kwamba hazita saini au
kuridhia Mkataba huo kama hautakuwa na mashiko, dhaifu au kwa namna moja
ama nyingine utakuwa unaingilia maslahi yao na masuala yao ya ndani
Tayari
washiriki wa mkutano huu wamekwisha anza jukumu la kupitia kipengere
kwa kipengere Rasimu ya Mkataba. Hatua hii inazipa fursa nchi wanachama
kuchangia maoni yao ya kuiboredha rasmu hiyo kwa ama kupunguza baadhi ya
vipengere, kuongeza na hata kuondoa kabisa baadhi ya vipengere.
No comments:
Post a Comment