Msanii
wa Muziki wa Kizazi,Kala Jeremiar akitoa shukrani zake kwa mashabiki
waliompigia kura na kumuwezesha kupata Tuzo tatu zikiwa ni Msanii Bora
wa Hip Hop,Mtunzi Bora wa Mashairi ya Hip Hop pamoja na Wimbo Bora wa
Hip Hop kwa kipindi chote cha Mwaka 2012/13.Kulia ni Msanii Shilole
aliepanda jukwaani Kumsindikiza.Hafla hii ya utoaji tuzo imefanyika Usiku wa kuamkia leo kwenye Ukumbi wa Mlimani City,jijini Dar es Salaam.
Msanii
Mkongwe wa Muziki wa Hip Hop hapa nchini ambaye sasa amepotea kidogo
kwenye Gemu hilo,Gwamaka Kaihula a.k.a King Crezy G.K akiwasalimia
mashabiki wake pindi alipopanda jukwaani kutoa tuzo ya Msanii Bora wa
Hip Hop.
DJ
Mseto toka Citizen TV ya Kenya akimuwakilisha mwanamuziki Jose
Chamilione baada ya kupata tuzo ya Wimbo bora wa Afrika Mashariki.
Ommy Dimpoz kwa Pozi aliondoka na tuzo tatu usiku wa kuamkia leo pale Mlimani City,jijini Dar
Mkurugenzi
wa Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),Kushila Thomas (katikati)
akiwa katika picha ya pamoja na kiongozi wa Bendi ya The Kilimanjaro
(wana njenje),Waziri Ally pamoja na Mwana FA baada ya kukabidhi tuzo ya
heshima kwa bendi hiyo,wakati wa hafla ya utoaji tuzo kwa wanamuziki
mbali mbali iliyofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye Ukumbi wa Mlimani
City,jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Konyagi,David Mgwassa (kushoto) akikabidhi tuzo ya heshima kwa
Picha kwahisani ya Jiachie Blog.
Redd's Miss Tanzania 2012,Brigit Alfred akikabidhi tuzo ya Msanii Bora wa K*** iliyokwenda kwa Bint Komando Lady Jay Dee.Anayeipokea tuzo hiyo ni Mumewe Lady Jay Dee,Ndugu Garder Habash.
G. Habash akizungumza kwa niaba ya Lady Jay Dee.
Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager,George Kabishe akitangaza mshindi wa tuzo Msanii Bora wa Bongo Flava.
Muwakilishi wa Msanii Diamond akishukuru kwa niaba yake.
Mtunzi Bora wa Mashairi ya Muziki wa Taarab ni Thabit Abdul na hapa akipongezwa.
Khareed Chokoraa akichukua tuzo ya Msanii Bora wa K***,ambayo ilikwenda wa Mkongwe Khadija Kopa.
Wawakilishi wa Isha Mashauzi wakipokea tuzo ya Msanii Bora wa K*** Taarabu kutoka kwa Mkurugenzi wa Aset,Baraka Msilwa.
Mrisho Mpoto na Ditto wakipokea tuzo ya Wimbo bora wenye vionjo vya asili.
Ben Pol akinyakua tuzo ya msanii bora wa kiume
Ben Pol akishuru mashabiki pamoja na Mama yake.
Tuzo ya Prodyuza bora wa Mwaka ilienda kwa Man Water.
Man Water akitoa shukrani
Wema Sepetu akitangaza mshindi wa Tuzo ya Video Bora ya Mwaka iliyokwenda kwa Ommy Dimpoz
No comments:
Post a Comment