Friday, February 22, 2013

LOWASSA ATOA UJUMBE KWA KIKWETE BAADA YA MATOKEO MABOVU YA FORM FOUR......SOMA ALICHOKISEMA HAPA

Written By Bongonewz Magazine on Thursday, February 21, 2013 | 4:51 PM

 
Waziri mkuu aliejiuzulu mh.Edward Lowassa,amemtaka raisi Kikwete aunde tume kuchunguza kilichopelekea matokeo mabaya ya form iv mwaka huu.Amesema tume itasaidia kubaini ni nini chanzo cha tatizo.

Wakati huo huo mh.Lowassa amemsifu kijana alimchora Messi na kusema kijana huyo ni intelligent.Amesifu uwezo wa kijana huyo kufanya hivyo.

Vile vile mh.Lowassa, ameitaka serikali kuongeza uwekezaji katika elimu kwani amesema tofauti na nchi zingine za Afrika mashariki Tanzania ndio ya mwisho kwa uwekezaji kwani inawekeza asilimia moja point sonething ya GDP katika elimu wakati Kenya ni asilimia tano na Rwanda kama sikosei amesema inawekeza mpaka asilimia 7 ya GDP katika elimu.Hivyo ametoa wito kwa serikali kuongeza uwekezaji katika elimu.

Mh.Lowassa pia amemsifu raisi Kikwete kwa kufanikiwa kaika maeneo mengine kama ujenzi wa bara bara,hospitali,zahanati na kwenye maeneo mengine na kumtaka ajielekeze zaidi katika elimu.Mh.Lowassa amerudia kauli yake na kusisitiza kuwa msimamo wake utabaki kuwa ni elimu kwanza na sio kitu kingine.

Miongoni mwa viongozi waliohojiwa ni pamoja na Zitto kabwe ambae mbali na kushauri mambo mbali mbali pia amewataka waziri wa elimu na naibu wake pamoja na katibu mkuu wa wizara ya elimu kujiuzulu.

No comments: