
Picha
Juu na chini ni Wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa wakiwapokea wageni
mbalimbali wakiwemo Mabalozi wa nchi mbalimbali, Wanafunzi wa vyuo
vikuu, Maprofesa, na wadau wa taasisi mbalimbali za Serikali na binafsi
waliohudhuria uzinduzi wa Ripoti ya Maendeleo Duniani 2013 uliofanyika
jijini Dar leo katika Hoteli ya Serena.(Picha na Zainul Mzige wa Mo Blog).
Mgeni
rasmi Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Peniel Lyimo akitoa hotuba
ya uzinduzi wa Ripoti ya Maendeleo Duniani ya mwaka 2013 - Kuchomoza kwa
Nchi za Kusini: Maendeleo ya Binadamu katika Dunia Anuwai akisema kwa
mujibu wa ripoti hii mwaka huu iaonekana kuwa Tanzania tumefanya vizuri
na kiwango chetu kimeongezeka kama ngazi mbili ikilinganishwa na ripoti
iliyopita.
Hata
hivyo amesema kwa bado kuna mikoa mingi ambayo unapopima maendeleo kwa
ujumla wake mikoa mingi ipo asilimia 20 hadi 30 ambapo hii inapima
ujumla wa maendeleo katika Jamii.
Bw.
Lyimo amesema kwa sasa serikali ina mipangp mizuri ya kuisaidia mikoa
hiyo, akitolea mfano kilimo kuwa kuanzia miaka ya 80 hatukuiangalia
vizuri tulikuwa na taasisi za kilimo, mashirika ya maendeleo ya viwanda
lakini katika kipindi hiki cha mageuzi tumepata matokeo mazuri.
Mratibu
Mkazi wa UN Tanzania Dkt. Alberic Kacou akizungumza wakati wa uzinduzi
wa Ripoti ya Maendeleo Duniani ya mwaka 2013 ikiainisha Kuchomoza kwa
Nchi za Kusini:Maendeleo ya Binadamu katika Dunia Anuwai ambapo amesema
sera kabambe, zilizotengenezwa vizuri zinaweza kufanya mafanikio ya
kimaendeleo ya binadamu kuwa endelevu katika miongo ijayo na kupanuka
kufikia nchi nyingi zaidi zinazoendela.
Lakini
pia Dkt. Kacou ameonya hatua za kubana matumizi zisizo na mtazamo wa
mbali, zaweza kushindwa kushughulikia hali ya kukosekana usawa, na
kukosekana kwa ushiriki wa maana wa jamii na kutishia maendeleo haya
kama viongozi hawatachukua hatua za kurekebisha.
Aidha
amesema baadhi ya mataifa yanayoongoza kwenye nchi za Kusini yanajenga
mwelekeo mpya wa kukuza maendeleo ya binadamu na kupunguza tofauti za
kimaisha kwa kuweka sera bunifu ambazo zinasomwa na kuigwa sehemu
nyingine duniani.
Baadhi
ya Wakuu wa mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa nchini
wakimsikiliza Dkt. Alberic Kacou (hayupo pichani) alipokuwa akisoma
hotuba yake kwenye hafla ya uzinduzi wa Ripoti ya Maendeleo Duniani 2013
iliyofanyika jijini Dar leo.
Mshauri
wa Uchumi wa UNDP Bw. Amarakoon Bandara akiwasilisha ripoti hiyo na
kuifafanua ambapo ameeleza kuwa Nchi za Kusini zinakabiliwa na
changamoto ambazo pia inazikabili nchi zilizoendelea za Kaskazini,
ikiwemo kuongezeka kwa idadi ya wazee, shinikizo kwenye mazingira,
tofauti za kimaisha katika jamii, kukosekana kwa uwiano kati ya
maandalizi ya kielimu na nafasi za kazi na umuhimu wa ushirikishwaji
umma na mengineyo, akisena hayo yanahitaji ufumbuzi wa kitaifa na
kimataifa ikiwa nchi zinazoendelea zinataka kuendeleza kasi yao ya
maendeleo.
Bw.
Amarakoon amesema Ripoti hiyo inaonya kuwa namba ya watu walio maskini
sana inaweza kuongezeka kufikia watu bilioni tatu ifikapo mwaka 2050,
labda tu kama hatua za pamoja kimataifa zitachukuliwa kuzuia maafa ya
kimazingira.
Mgeni
rasmi Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Peniel Lyimo akikata utepe
kuzindua rasmi wa Ripoti ya Maendeleo Duniani ya mwaka 2013 ikiainisha
Kuchomoza kwa Nchi za Kusini:Maendeleo ya Binadamu katika Dunia Anuwai
akiwa na Mratibu Mkazi wa UN Tanzania Dkt. Alberic Kacou katika hafla
hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Sasa imezinduliwa rasmi.
Mmoja wa mabalozi akiperuzi Ripoti ya Maendeleo Duniani 2013 baada ya kuzinduliwa rasmi.
Ripoti
ya mwaka 2013 inasema kuchomoza kwa Nchi za Kusini ni changamoto kwa
taasisi duniani kubadilika na kunaonyesha njia mpya ambazo nchi na
maeneo yanaweza kufanya kazi pamoja kukabiliana na changamoto
zinazofanana.
Wakati
taasisi kongwe haziendi na mabadiliko, taratibu mpya zinatokea, ikiwamo
mitandao mipya ya ushirikiano ya kitaifa na kimataifa zikiwemo jumuiya
za kibiashara, jumuiya za kiulinzi, benki za maendeleo na makubaliano ya
nchi kwa nchi.
Baadhi ya Waheshimiwa mabalozi mbalimbali wanaoziwakilisha nchi zao nchini wakishuhudia uzinduzi wa Ripoti hiyo.
Mwakilishi wa UN Women Tanzania Bi. Anna Collins-Falk.
Mwanafunzi
wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Mollel Raphael Leckshon akitoa maoni
yake juu ya Ripoti ya Maendelo ya Dunia 2013 iliyozinduliwa rasmi leo
jijini Dar es Salaam.
Prof. Delphin Rwegasira kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam akichangia maoni yake baada ya ripoti hiyo kuwasilishwa.
Wageni
waalikwa na baadhi ya wafanyakazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa
nchini katika uzinduzi wa Ripoti ya Maendeleo Duniani 2013.
Mkurugenzi
Mkazi wa UNDP nchini Tanzania Bw. Phillipe Poinsot akitoa neno la
shukrani kwa wageni waalikwa waliohudhuria uzinduzi wa ripoti hiyo.
Mratibu
Mkazi wa UN Tanzania Dkt. Alberic Kacou akibadilishana mawazo na baadhi
ya waheshimiwa mabalozi baada ya uzinduzi wa Ripoti ya Maendeleo ya
Dunia 2013.
Sangita
Khadka wa Ofisi ya RCO (kushoto) na Stella Vuzo wa Kitengo cha habari
cha Umoja wa Mataifa (UNIC) baada ya uzinduzi wa Ripoti ya Maendeleo ya
Dunia 2013 iliyozinduliwa rasmi jijini Dar leo katika Hoteli ya Serena.
No comments:
Post a Comment