Wanasema viboko vitasaidia sana vijana wetu kushinda
mitihani na kutokufeli hata kidogo kwa hiyo tuwachape sana. Wizara ya elimu
badala ya kusambaza vitabu, vifaa vya maabara nk sasa isambaze viboko
mashuleni. Wafanya biashara wapewe tenda za kusafirisha “njiti” mashuleni kwa
ajiri ya kuwachapa vijana wetu ili washinde mitihani yao.
Sijui kama utafiti umefanywa juu ya unjitishaji wanafunzi
ili washinde mitihani au ni wale waliopata elimu kwenye mfumo wa kikoloni wa
kuchapwa wanataka na watoto wao wachapwe ili wakione cha moto waliokipata
wazazi wao kutoka kwa wakoloni na walimu wao waliofanya kazi kama wakoloni.
Nikiwa shule ya sekondori nililiichukia somo la fizikia kwa
sababu tatu ambazo ni; mwalimu wa somo hilo kufundisha huku akivuta sigara darasani,
matusi kwa wanafunzi pamoja na kuchapa viboko vilivyopitiliza kwa wanafunzi
waliokosea, niliamua kuacha somo hili kama njia ya kuzikimbia adha za mwalimu
huyu, Je viboko vitafaulisha kweli?
Walimu waliochanganyikiwa kwa mishahara midogo, makazi duni
na mazingira magumu ya kazi yanayotokana na upigaji kura wa wazazi wa wanafunzi
wao na wanafunzi wenyewe ukiwaruhusu kupiga viboko kama njia ya ufaulishaji
katika ugiligili (frustrations) hizo si watawatwanga vijana wetu mpaka watokwe
damu?
Shule zinazofaulisha vizuri wanafunzi wao katika mataifa
yaliyoendelea na hata shule binafsi hapa nchini kama seminari, Academy nk, wanawachapa wanafunzi zaidi kuliko hizi
za kata au wana Vitabu vya kutosha, maabara nzuri, maktaba, madarasa bora huku
wakiwapa walimu wao mazingira mazuri ya kazi? Kuna jamaa yangu ni mwalimu wa
kiingereza katika shule moja ya binafsi, huyu bwana mshahara wake ni mzuri na
huduma nyingine za kibinadamu zimeboreshwa, ndivyo matokeo y a somo lake
yanavyokuwa mazuri kila mwaka.
Kama viboko nisuruhisho basi tuwachape wote sio
watoto/wanafunzi tu. Tuwachape mawaziri wanaoshindwa kutimiza majukumu yao,
tuwachape wabunge wanaosinzia bungeni, tuwachape mafisadi, tuwachape
wafanyakazi wanaochelewa kazini, tuwachape maaskari wanaokula rushwa, tuwachape
akina mama wanaoshindwa kunyonyosha watoto wao, tuwachape wanaume/wanawake
wanaotoka nje ya ndoa.
Tuwachape viongozi wa dini wanaowatongoza waumini wao kwa
kutumia sadaka za Mungu, tuwachape makandarasi wabovu, tuwachape madereva
wanaovunja sheria za usalama barabarni, tuwachape wanasiasa wanaoshindwa kutimiza
ahadi zao, tumchape kila mtu. Kwanini viboko viwe kwa ajili ya wanafunzi/na
watoto pekee na sio wengine wanaofeli kutimiza majukumu yao? Tumchapee kila mtu
harafu tusiwe na miudombinu mashuleni, vijana wetu watashinda kwa miujuza ya
kiboko nakwambia.
No comments:
Post a Comment