Monday, May 27, 2013

KAMA HUKUPATA NAFASI YA KUONA PICHA ZA KILICHOJIRI MAHAKAMANI SIKU RAMA MLA WATU ALIPOACHIWA HURU, BASI HUU NDO MDA WAKO KUZITAZAMA HAPA

Na Richard Bukos
HUKUMU ya kuwaachia huru washitakiwa waliokuwa wakikabiliwa na kesi ya mauaji, Ramadhan Seleman Mussa ‘Rama Mla Watu’ na mama yake, Khadija Ally Seleman imeibua vicheko na vilio katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Ijumaa iliyopita.
Ramadhan Seleman Mussa ‘Rama Mla Watu’ akiwa na furaha baada ya kuachiwa huru.
Huku Ijumaa Wikienda likifuatilia hukumu hiyo hatua kwa hatua, hali hiyo ya taharuki ilitokea mara baada ya jaji wa mahakama hiyo, Rose Temba kuwaachia huru washitakiwa hao na kuibua sekeseke hilo huku mayowe ya vicheko na vilio vikitawala kutoka pande mbili zilizokuwa zikifuatilia kesi hiyo.
Ikumbukwe kwamba kijana Rama na mama yake walikuwa wakishitakiwa kwa kosa la mauaji ya mtoto Salome Yohana yaliyotokea mwaka 2008.
Wakati upande wa familia ya Rama ukigubikwa na furaha baada ya kuachiwa huru, upande wa wazazi wa Salome uliangua vilio kuonesha kutoridhishwa na hukumu hiyo.
Mama mzazi wa Rama, Khadija Ally Seleman.
Kabla ya hukumu, Jaji Temba alipitia mwenendo mzima wa kesi hiyo na kubaini kwamba mshitakiwa namba moja (Rama) alionekana kuwa na hatia na kuzitaja sababu zilizomtia hatiani kuwa ni kukamatwa na kichwa cha mtoto huyo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na kiwiliwili chake kukutwa kwenye tundu la choo nyumbani kwa washitakiwa hao, Tabata jijini Dar.
Hali kadhalika, mwili huo wa Salome ulikuwa umeviringishwa na fulana ya Rama.
Jaji Temba alisema sababu nyingine iliyowatia hatiani Rama na mama yake ni maelezo ya Rama kuwa mama yake ndiye aliyemuua Salome kwa kumkata kichwa kwa kutumia shoka na kumpa kichwa hicho ili akipeleke kwa shangazi yake anayefanya kazi Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Jaji Temba alisema licha ya ushahidi huo, alipitia maombi ya wakili wa washitakiwa hao, Yusuph Shekha aliyeomba mteja wake, Rama akapimwe akili.
Mama mzazi wa marehemu Salome, Pendo Dustan.
Baada ya Rama kupelekwa katika Hospitali ya Mirembe mkoani Dodoma, jaji huyo alisema ripoti kutoka kwa daktari, Mndeme Erastus ilionesha kuwa wakati Rama akitenda kosa hilo alikuwa na matatizo ya akili.
Ripoti hiyo ilimfanya jaji huyo kuwafutia mashitaka washitakiwa hao kwa kuwa, mshitakiwa wa pili aliingizwa hatiani kutokana na maelezo ya mshitakiwa wa kwanza.
Baada ya kutoa maelezo hayo, jaji huyo aliwaachia huru Rama na mama yake lakini aliamuru Rama awekwe chini ya uangalizi kwenye hospitali ya wahalifu ya Isanga mkoani Dodoma hadi akili yake itakapotengemaa.
Baba wa marehemu Salome, Yohana Majana.
Kufuatia taarifa ya hukumu hiyo, ndugu wa washitakiwa walikuwa wakishangilia huku Rama akisubiriwa mtaani wakati upande wa wazazi wa Salome ulikuwa ukihuzunika na ‘kumaindi’.
Kwa upande wa familia ya Salome, waliokuwepo mahakamani hapo ni mama mzazi, Pendo Dustan na baba wa marehemu, Yohana Majana na Furaha Musa ambao walionekana kupigwa na fadhaa na kuangua vilio mahakamani hapo huku wakitafuta njia ya kukata rufaa.
“Jamani mwanangu, roho inaniuma sana! Kibaya muuaji wake leo ameachiwa, lazima tukate rufaa,” alisema mama wa marehemu huku akilia kwa kwikwi.
Anti wa Salome.
“Ina maana kesi ya Salome ndiyo imeishia hivyo, masikini Salome uuuwii,” alisikika mwanamke mwingine huku akiangua kilio.
Hali hiyo iliwafanya askari kuingilia kati na kuwatoa nje watu wote.
Watu wengi wamekuwa wakimsubiri Rama nyumbani kwao Tabata kwa lengo la kutaka kumshuhudia ‘live’.

No comments: