Thursday, August 8, 2013

SABABU MBILI ZILIZOMFANYA MADAM RITA AIHAMISHIE BONGO STAR SEARCH TBC1


Epiq Bongo Star Search ya mwaka 2013 haitaoneshwa tena kupitia ITV.  Mwaka huu shindano hilo la kusaka vipaji vya kuimba litakuwa likioneshwa  kupitia TBC1.


Kupitia Facebook, Rita Paulsen aka Madam Rita ambaye ni  mwanzilishi na jaji mkuu wa shindano hilo ametoa sababu mbili za  kuhamisha matangazo hayo kutoka ITV hadi TBC1.


“Baada ya kusoma maoni yenu, ningependa kufafanua sababu mbili za  kurusha Epiq Bongo Star Search 2013 kupitia kituo cha Televisheni cha  TBC1.


Kwanza kabisa ni sababu za kibiashara ndio zimepelekea kipindi cha  EBSS kurushwa kupitia TBC1 na sababu ya pili ni kwamba baada ya kwenda  kidigitali, TBC1 sasa inapatikana kwenye ving’amuzi karibia vyote  vikiwemo Star Times, DSTV na Zuku.”

No comments: