Wednesday, January 30, 2013

BUNGE LAUNDA KAMATI MAALUMU KWENDA MTWARA


Spika wa Bunge bi Anne Makinda amesema Bunge limeunda Kamati Maalumu kwenda mkoani Mtwara kutafuta suluhu kuhusu suala la nishati ya gesi, iliyopatikana mkoani humo.

Spika Makinda ameyasema hayo wakati akiahirisha kikao cha Bunge kilichoanza leo Mkoani Dodoma.

Spika amesema matokeo ya Kamati hiyo Maalumu yatawasilishwa kujadiliwa Bungeni.

Iddi Maalim wa TBC anaripoti katika taarifa iliyosomwa saa saba mchana ifuatavyo:

Bunge sasa linaunda Kamati ambayo itakwenda Mtwara, kuwasikiliza Wananchi halafu ndani ya kikao hiki –mkutano huu unaofanyika– Kamati ya Bunge itakuwa imekwenda Mtwara, itawasikiliza Wananchi, italeta masuala ambayo yanazungumzwa kule Mtwara kisha yatajadiliwa.

Hili alikuwa analizungumza baada ya kusema kuwa amepokea vikaratasi na maombi mengi kwamba Bunge lijadili suala la Mtwara, gesi kama suala ambalo ni la dharura.

Lakini akasema kwamba, ile hoja si ya dharura na akaeleza pia ukweli kwamba Wabunge ambao wanasema lijadiliwe kama suala la dharura wengi wao hawalifahamu kwa undani, kwa hiyo badala ya kujadili jambo ambalo hawalifahamu kwa undani, ni afadhali ataunda kamati ambayo itakwenda Mtwara ikirudi itakuja na majibu, na mapendekezo ya Wananchi na ndipo Bunge litajadili ndani ya Mkutano huu wa kumi.

BIASHARA HARAMU YA WASICHANA KUTOKA TANZANIA- ZANZIBAR NA HATIMAYE UARABUNI YAZIDI KUOTA MIZIZI


Biashara ya binadamu imeibuka kwa kasi nchini na kutishia usalama wa nchi kutokana na watoto wenye umri kati ya miaka 8-15 baadhi yao wakiwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari  kusafirishwa kinyemela kwenda katika nchi za Uarabuni.

Uchunguzi wa kina uliofanywa na NIPASHE kwa takribani wiki mbili, umebaini kuwa biashara hiyo imeibuka kuanzia Desemba mwaka jana na imeshika kasi Januari mwaka huu na wanaosafirishwa  wengi ni watoto wa kike kutoka mikoa mbalimbali nchini. Wapo wachache wa kiume pia.

Kamanda wa Polisi Kikosi cha Maji, Mboje Kanga, alipoulizwa na NIPASHE alithibitisha kupata taarifa za kuwapo kwa biashara hiyo ingawa alisema kuwa hana takwimu za watoto ambao wamekamatwa wakitaka kusafirishwa.

Tatizo la kusafirisha watoto lipo, lakini nina watu ambao wanashughulikia suala hilo pale bandarini, nitafute kesho (leo) nitakupa takwimu zote kuhusiana na biashara hiyo baada ya kuwasiliana na watu wangu.

Uchunguzi zaidi  umebaini kuwa mikoa ambayo watoto hao wananunuliwa na mawakala maalum kabla ya kusafirishwa kupelekwa nchi za Uarabuni kufanya kazi mbalimbali zikiwamo za ndani ni Mtwara, Lindi, Manyara, Pwani, Tabora, Ruvuma, Tanga na Shinyanga.

Taarifa zinaonyesha kuwa mawakala hao wakishafanikiwa kuwapata watoto hao kutoka katika mikoa hiyo huwapeleka Jijini Dar es Salaam na baadaye kusafirishwa kwa usafiri wa majini kutoka Bandari ya Dar es Salaam kwenda Zanzibar.

Uchaunguzi umebaini kuwa watoto hao wakifikishwa Zanzibar hukutana na watu maalum ambao huwapokea na kufawanyia mipango ya kuwasafirisha kwa usafiri wa ndege au wa majini kwenda Uarabuni ambako hutumikishwa katika kazi mbalimbali.

Mawakala hao wakishafanikiwa kuwasafirisha kutoka Bandari ya Dar es Salaam, hulipwa wastani wa Dola za Marekani 5,000 (Sh. milioni 8) kwa kila mtoto wanayefanikisha kumvusha kutoka Tanzania Bara kwenda Zanzibar.

Kwa mujibu wa uchunguzi huo, ili kuhalalisha safari za kuwasafirisha watoto hao, mawakala wanakula njama na baadhi ya wenyeviti wa serikali za mitaa kwa kuandika barua zinazoelezea sababu za watoto hao kwenda Zanzibar.

Barua hizo ambazo imebainika ni za kughushi, nyingi zinaandikwa na kupigwa mihuri ya wenyeviti wa serikali za mitaa wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke, jijini Dar es Salaam.

Sehemu ya barua hizo ambazo NIPASHE ilifanikiwa kuona nakala yake ianasomeka:

Tunaomba mtoto huyu asitiliwe mashaka (shaka) bali apewe ushirikiano, anasafiri kwenda Zanzibar kusalimia ndugu zake walioko huko ambao watampokea.

WABUNGE WALIO CHOMEWA NYUMBA ZAO HUKO MTWARA WAANGUA KILIO


WABUNGE waliochomewa nyumba na mali zao katika vurugu zilizotokea Mtwara juzi; Anna Abdallah na Mariam Kasembe, jana waliangulia vilio walipotakiwa na mwananchi  kuzungumzia tukio hilo.

Nyumba za wabunge hao wa Viti Maalumu na mali zingine kadhaa za taasisi mbalimbali, ni miongoni mwa vitu vilivyoharibiwa katika vurugu hizo ambazo pia zilisababisha vifo vya watu wanne wilayani Masasi.

Akizungumza kwa huzuni,  Anna alisema hajui sababu za uharibifu huo, hasa ikizingatiwa mwenyewe amekuwa huko kwa karibu siku tatu na hakuona dalili za uhasama wowote dhidi yake.

Anna ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Korosho alisema: “Nina siku ya tatu hapa Masasi na nimeshiriki mkutano wa halmashauri kwa mwaliko na wakati wote, sikuhisi chochote hivyo siwezi kujua sababu ya chuki iliyofanya nyumba yangu ichomwe moto,” alisema.

Alipotakiwa aeleze hali ilivyokuwa, alisema, “Wavamizi hao walipora kila kitu nyumbani kwangu yakiwamo mapazia, kabla ya kumwaga petroli kila chumba na kuwasha moto.”

Aliendelea kueleza,” Kila kitu kiliteketea. Inatia uchungu kwani nyumba hiyo niliijenga kwa kudunduliza fedha kidogo kidogo nikiwa mkuu wa mkoa.”

Anna alisema, kundi hilo la vijana lilivamia nyumbani kwake saa 4:00 asubuhi na kuanza kupora mali kwa kupita chumba kimoja baada ya kingine.

“Hali si nzuri. Kila kitu kimeibwa na nyumba imechomwa moto, hakuna kilichobaki. Walichukua kila kitu na itanichukua muda mwingi kujua thamani halisi ya hasara iliyopatikana,” alisema.

Kauli ya Kasembe
Naye Kasembe alipokea simu ya mwandishi wa habari hii kwa kilio na kuikata huku akisema, “Jamani niacheni… Mwenzenu naumia…!”


Alipopigiwa tena baadaye, alisema anashangazwa na tukio hilo ambalo limemfika bila kutarajia na kumtia hasara kubwa.

“Wamepora kila kitu katika nyumba na kuichoma moto, sijui atakuwa nani huyu, kwani sina tatizo na wapiga kura wangu na sina mgogoro na mtu yeyote. Nashindwa hata kuhisi nani kafanya uchochezi,” alisema Kasembe.

Alisema wakati wa vurugu hizo, ndugu zake akiwamo mama yake, walikimbia na kwenda kujihifadhi hotelini, lakini mpaka sasa hawajui wataishi vipi baada ya nyumba hiyo kuteketezwa kwa moto.

“Jana wanafamilia walilala hotelini na leo tupo nje ya gofu la nyumba yangu ambayo imeteketea kabisa kwa moto, tunasubiri majaaliwa mengine, lakini nimechanganyikiwa kwa kweli na sijui ni kitu gani hiki, siamini,”alisema.

Polisi waeleza uharibifu
Watu 44 wanashikiliwa na polisi wilayani Masasi kufuatia vurugu hizo.


Kamanda wa Polisi Mkoa  wa Mtwara, Maria Mzuki alisema watu hao wamekamatwa kwa wakituhumiwa kujihusisha na vurugu hizo zilizosababisha uhalibifu mkubwa mali.

USHAHIDI WA PICHA TATU ZA LULU BAADA YA DHAMANA KUKAMILIKA, MUDA MFUPI KABLA YA KUINGIA URAIANI

Lulu na mama yake mzazi wakilia baada ya kukutana nje ya Mahakama, Lulu amechiwa huru na Mahakama leo january 29 2013 mchana, pembeni ni mwigizaji Dr. Cheni ambae amekua karibu na familia ya Lulu kwa muda mrefu sana.
Lulu akiingia kwenye gari.
Machozi ya furaha.
Picha zote zimepigwa na habarimpya.com

DONDOO MUHIMU KUHUSU KIKAO CHA KUTAFUTA SULUHU KILICHOENDESHWA NA WAZIRI MKUU HUKO MTWARA



Waziri Mkuu Mizengo Pinda akisisitiza jambo wakati wa kikao chake na Baadhi ya Viongozi wa Vyama vya siasa na viongozi wa Asasi mbalimbali kuhusu mgogoro wa gesi kwenye ukumbi wa VETA mjini Mtwara Januari 27, 2013
------------------
Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda yupo Mkoani Mtwara akikutana na makundi ya wadau mbalimbali wa mkoa huo ili kusikia kutoka kwao mawazo, michango na dukuduku zao kuhusu mradi wa gesi asilia.

Imeripotiwa kuwa Waziri Mkuu angekutana na wanahabari baadaye leo saa 9 alasiri ili kutoa mjumuisho wa maongezi yake...
 Taarifa mpya zitawekwa hapa punde zitakazopatikana. Kwa sasa, tafadhali sikiliza rekodi ya kipindi cha Amka na PRIDE FM radio, kilichozungumzia muhtasari wa yaliyojiri katika kikao cha jana kati ya Waziri Mkuu na Wadau.

Sikiliza Mtwara na Waziri Mkuu - PRIDE FM

--------------
UPDATES/TAARIFA MPYA
za ziara ya Waziri Mkuu

Waziri Mkuu alikuwa akutane na Waandishi leo saa tisa alasiri. Kutokana na kikao kirefu cha madiwani wa Manispaa ya Mtwara/Mikindani na Mtwara vijijini pamoja na kikao cha wafanyabiashara, majumuisho ya ziara ya Mtwara atayatolea ufafanuzi kesho.

Dondoo muhimu:

  • Kwa ufupi wajumbe wengi wamekataa bomba la gesi lisiende Dar
  • Wamemkataa Mkuu wa Mkoa na kumtaka Waziri Mkuu aondoke naye
  • Wajumbe (Madiwani ) kumpinga kwa kauli moja  Hawa Ghasia kwa kile kilichosemwa kutumia mamlaka  kutoa kauli za uongo kuhusu Mtwara Vijijini kuunga mkono suala la gesi iende Dar madiwani waMtwara vijijini. Wamesema hawakushirikishwa.
  • Mzozo wa viwanja baina ya Madiwani na Mkuu wa Wilaya
  • Waziri Mkuu ametumia mbinu ya kisiasa kuwashawishi Wadau kuwa bomba liende Dar
  • Wajumbe wameondoka kwa shingo upande kwa kukubali kutokubaliana na Waziri Mkuu
  • Kikao kinafanyika chini ya ulinzi Mkali wa FFU, JWTZ na UwT (Usalama wa Taifa)
  • Hawa Ghasia arudishwa Uwanja wa Ndege, JKNIA asije Mtwara kwani anaweza kuchafua hali ya hewa
  • Polisi wanadai Meya anataka kuwachonganisha na jamii/wananchi kutokana na kauli yake ya kusema wao ndio chanzo cha vurugu

Tuesday, January 29, 2013

MKE WA MTU AVUA NGUO HADHRANI BAADA YA POMBE KUPANDA KICHWANI....



KITUKO cha aina yake kimejiri Jumamosi iliyopita ndani ya Ukumbi wa Meeda Sinza jijini Dar wakati Bendi ya Extra Bongo ‘Wazee wa Kizigo’ ilipokuwa ikitumbuiza

Katika onesho hilo, mwanamke mmoja anayedaiwa kuwa ni mke wa mtu alifanya kitendo cha aibu baada ya kusaula nguo zake zote na kubakia na nguo za ndani.

Katika onesho hilo, Extra Bongo ilikuwa ikiwashindanisha mashabiki wake kucheza staili yao ya Kizigo na washindi kujinyakulia zawadi za fedha.


Wakati bendi hiyo inayoongozwa na ‘Kamarade’ Ally Choki ikitoa burudani, ghafla mwanamke huyo  alivamia jukwaa na kuanza kucheza kwa staili aliyokuwa akiijua mwenyewe.



Mpigapicha wa amani  alipojaribu kumpiga picha dada huyo alihamaki na kumjia juu huku kumtishia kumvunjia kamera yake huku akidai kuwa yeye ni mke wa mtu, hivyo hapaswi kupigwa picha.

“Mimi ni mke wa mtu ukifanya mchezo nitakutolea laana,”
alisema mwanamke huyo huku akizishika nguo zake na kuanza kuzitoa mwilini mwake  moja baada ya nyingine.


Wakati mwanamke huyo akiendelea na zoezi lake la kusaula nguo, alijitokeza dada mwingine ambaye  aliambatana naye pamoja ukumbini hapo na kumwita  kwa jina la wifi.


“Wifiii…, wifiii…, weee wifii pombe gani hizo, usivue nguo, usifanye hivyo ni aibu,  itakuwaje kaka akiziona hizo picha magazetini?” alisema dada huyo aliyedaiwa kuwa ni wifi mtu lakini pamoja na kumpigia kelele hizo haikusaidia kumzuia  mwanamke huyo mcharuko kusaula nguo zake.

Baada ya kuombwa sana na wifi yake, mwanamke huyo alivaa nguo zake na kuendelea na burudani hadi mwisho.


Haikufahamika mara moja kama mwanamke huyo alifanya  kitendo hicho kutokana na pombe au hasira za kupigwa picha.

PEOPLE`S POWER

KIKAO CHA DHARURA CHA BARAZA KUU LA CHADEMA KATIKA PICHA


 Mbunge wa Ubungo John Mnyika akitete jambo na Katibu Mkuu wa Chadema Dk. Willbroad Slaa (kulia) wakati wa Kikao cha dharura cha Baraza Kuu la Chadema kilichofanyika jijini Dar es Salaam, leo. (Picha na Habari Mseto Blog)
 Mbunge Kigoma, Zitto Kabwe akiwasikiliza kwa makini wajumbe wa kikao cha dharura cha Baraza Kuu la Chadema kutoka mkoa wa Mtwara.
 Mbunge wa Ubungo, John Mnyika akiwa amepozi na baadhi ya wajumbe.
 Baadahi ya wabunge wa Chadema wakiwa katika kikao hicho.

 Kazi imeanza
 Muasisi wa Chadema, Edwin Mtei akiingia katika ukumbi wa mkutano huku akifuatana na Mwenyekiti wa Chadema, Freema Mbowe.
 Wajumbe wa mkutano.
 Katibu Mkuu Dk. Willbroad Slaa akizungumza katika mkutano huo.
 Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe akifungua mkutano huo
 Wajumbe wa Kamati Kuu.
 Peoples Power
 Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe akimkabidhi kadi ya uanchama wa chama hicho aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu Bara wa Chama cha NCCR-Mageuzi, Clemence Tara baada ya kujiunga na chama hicho.
 Pokea katiba ya chama cha Chadema
 Bidhaa mbalimbalio zenye nembo ya Chadema zikiuzwa

BREAKING: PICHA 8 ZA LULU MAHAKAMANI LEO JAN 28 PAMOJA NA MAELEZO YA MASHARTI YA DHAMANA YAKE.


Lulu akiwa anaingia Mahakamani leo january 28 2013 akiwa na shauku ya kupata dhamana.
Mahakama kuu leo imetangaza dhamana ya mwigizaji Lulu lakini iwapo atatimiza masharti aliyopangiwa ambayo ni pamoja na kuwasilisha hati yake ya kusafiria, kutosafiri nje ya Dar es salaam, kujiwakilisha au kuripoti mahakamani kila siku ya kwanza ya kila mwezi pamoja na wadhamini wake wawili ambao kila mmoja adhamini kwa shilingi milioni 20 za kitanzania.
Upande wa familia ya Lulu umesema masharti yote yaliyotajwa wanaweza kuyatimiza leo leo hivyo wanasubiri tu jibu la msajili ambae ndio anatakiwa kuhakikisha hayo masharti yametimia kisha ruhusa ya kumkabidhi Lulu kwa familia yake itolewe.
Taarifa za ndani ni kwamba uwezekano wa Lulu kuachiwa upo kuanzia january 29 2013 ambayo ni kesho kwa sababu kuna watumishi wawili wa serikali ambao wapo kikazi mkoani Pwani na ndio walitakiwa kutia saini dhamana ya Lulu wakiwa ni sehemu ya masharti.
.
.
.
.
Hapa ni wakati alipocheka sana pale mwandishi mmoja wa kike ambae pia alikua akimpiga picha alipokua akimlainisha Lulu kwa maneno baada ya mwigizaji huyo kuficha uso wake alipokua akipigwa picha, alisema alikua anaumizwa macho na mwanga wa kamera.
.
.
Mama mzazi wa Lulu ni mwenye nguo nyeupe na nyeusi.
Unaweza kumsikiliza mwigizaji Dr Cheni hapo chini, ni mmoja ya watu waliokaribu na familia ya Lulu na ameshirikiana nayo kwa muda mrefu sana kwenye hii kesi ikiwemo kufatilia mawakili, kushughulikia dhamana na mengineyo.

Monday, January 28, 2013

VURUGU ZA MTWARA



Taarifa za redio mbao ambazo hazijathibitishwa na Mamlaka yeyote hadi hivi sasa ni kwamba wananchi wanaendelea kufanya uharibifu mkubwa huko ambapo naambiwa wamevamia gereza wakafungulia wafungwa na kisha kupiga moto gereza. 

Polisi wamezidiwa na wamejifungia kituoni wanarusha mabomu yao tokea huko walikojificha maana nje hakutamaniki. Na wameshateketeza nyumba ya mama Anna Abdallah.
 
Taarifa hizi ni kwa mujibu wa Blog ya MTWARA KUMEKUCHA …...

Updates
  • Kikao cha dharura cha kamati ya ulinzi na usalama kinaendelea kwa kuwashirikisha maafisa wa polisi na maafisa usalama waliotoka Dar es Salaam kuongezea nguvu.
  • Maaskari na makachero wamewasili Mtwara leo asubuhi na helkopta kuongezea nguvu.Maaskari na makachero wawasili  Mtwara leo asubuhi na helkopta kuongezea nguvu.
  • Hosteli ya wanafunzi wa chuo cha Utumishi maeneo ya Kiyangu B Mtwara yakoswa koswa kuchomwa moto kwa kile kinachodhaniwa kuwa na uhusiano na Hawa Ghasia mpaka sasa wanafunzi hawana mahala pa kukaa. 
  • Kituo kidogo cha Polisi Cha Shangani mkoani Mtwara nacho chakoswa na moto. Ofisi ya Afisa Mtendaji Nkanaledi mkoani Mtwara nayo yavunjwa.
  • Wananchi wamechoma moto mahakama ya Mwanzo na kuvunja vioo vya nyumba za waheshimiwa Hawa Ghasia (Waziri, TAMISEMI) na ya Mohamed Sinani (Mwenyekiti wa CCM Mkoa) zilizopo mtaa wa Sinani.
  • Wakiwa katika mahakama ya mwanzo, Polisi walizingirwa na vijana waliokuwa wamebeba mawe na kufunga barabara zote za kuingia na kutoka Kituo Kikuu cha Mabasi na eneo la Soko Kuu, licha ya kufyatua hewani mabomu ya machozi. 
  • Baadhi ya barabara za zimezibwa kwa kuchomwa matairi ya gari, na kuongeza hofu kwa wananchi.
  • Hali imeshakuwa mbaya Masasi taarifa zilizotufikia punde wamechoma eneo linaloitwa loliondo, ofisi za elimu na ofisi ya trafiki, inasemekana jamaa wameshavamia ofisi za halmashauri wengine wako njiani nyumbani kwa mama Ana Abdala, hapa Mtwara  mjini maduka yote eneo la soko kuu na stendi yamefungwa hakuna huduma, huko Newala , leo kuna mkutano mkubwa mchana huu wa kumkataa George Mkuchika.
  • Vurugu zahamia wilaya ya Masasi mkoani Mtwara Nyumba ya Mbunge wa Masasi nayo yateketezwa kwa Moto hivi sasa...Madereva Bodaboda waandamana ...Vurugu zashamiri Mabomu Kibao..Hali ni tete
Askari auawa
Na taarifa zaidi kutoka Masasi zinaeleza kuwa askari wa upelelezi Masasi aliyejichanganya katika vurugu wananchi walimshitukia akiwapiga picha, akashambuliwa na kuuliwa. Askari huyo inaelezwa amekutwa na bastola mbili. Taarifa zaidi baada ya kuthibitishwa tutawaletea

MTWARA NA GESI IMEKUWA NOMAA

UPDATE ZA MTWARA;. WALIOFARIKI WAFIKA 9, VIONGOZI WA SERIKALI WAWASILI


IDADI ya watu waliouawa katika vurugu za wilaya ya Masasi,mkoani Mtwara imeongezeka na kufikia Tisa kutoka saba walioripotiwa awali.

Mmoja aliyekuwa majeruhi na kulazwa hospitali ya misheni ya Ndanda ameripotiwa kupoteza maisha yake.

Ndugu wa karibu wa marehemu amemthibitishia mwandishi  kuwa ndugu yao amefariki leo saa 9 usiku akiwa anpatiwa matibabu hospitalini.

Mchana wa leo, mwendesha bodaboda mmoja ameuawa kwa kupigwa na vitu vinavyosadikika kuwa ni risasi za moto na kupoteza maisha papo hapo. Wananchi wamedai polisi wakiwa katika gari walimminia risasi kijana huyo aliyekuwa anaendesha pikipiki yake. Haya ni mauaji ya kwanza kutokea kwa polisi kuua watu wengi kwa risasi za moto, hali inayoitia doa Serikali.

Tayari Waziri wa Mambo ya Ndani, Emanuel Nchimbi amewasili mkoani Mtwara akiambatana na Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP, Saidi Mwema, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi (JWTZ) Davis Mwamunyange. Habari zinasema kuwa viongozi hao watafaya kikao na viongozi wa Mtwara na badaye kwenda Masasi kushuhudia hali ilivyo.

Hata hivyo kuna habari kuwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda atawasili kesho mjini Mtwara, kufuatia vurugu zinazoendelea ambazo zinachagizwa na kupinga gesi kupelekwa Dar es Salaam.

Endelea kufuatilia 

Tuesday, January 22, 2013

Mungu ailaze mahala pema roho ya Marehemu Lydia

MWANACHUO WA SAINT JOHN, DODOMA AUAWA KIKATILI

JESHI la polisi mkoani Dodoma limeshutumiwa kwa kushindwa kuimarisha ulinzi katika baadhi ya maeneo mkoani humo hatua inayodaiwa kuchangia kuaawa kinyama kwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Saint John Lidya Leo Mzima na watu wasiojulikana.

Marehemu Lidya mwenye umri wa miaka 57 anadaiwa kuuawa siku ya jumapili hii majira ya saa nne za usiku pembezoni mwa maeneo ya chuo hicho chenye wanafunzi 5500
akiwa anarejea nyumbani baada ya masomo ya jioni.

Ni simanzi,vilio,huzuni na majonzi katika vyunga vya chuo hiki kufuatia tukio hili la kusikitisha ambalo linadaiwa kuyaweka katika mashaka na wasiwasi mkubwa maisha ya wanafunzi hawa.


Licha ya kulitupia lawama jeshi la polisi baadhi ya mashuhuda wanadai kuwa baada ya kufikwa na mkasa huo uliositisha safari ya maisha yake mwili wa marehemu Lidya uliharibiwa vibaya na mnyama asiyejulikana kwa kunyofolewa macho,masikio,pua,mguu na viuno vingine.


Prof.Gabriel Mwaluko ni makamu mkuu wa Chuo na Karimu Meshack ni afisa habari ambao kwa pamoja wanaelezea kilichorjiri.


Kutokana na shutuma za uzembe dhidi ya jeshi hilo, Kamanda wa mkoa ACP David Misime anawataka wakazi wa mkoa huo kuimarisha ulinzi shirikishi kwa lengo la kuwabaini wahalifu.


Wakati huo huo Kamanda Misime anasema msako mkali umeanza wa kuwatia nguvuni waliohusika na ukatili huo ili waweze kufikishwa kwenye mikono ya sheria kwa ajili ya hukumu.


Tuesday, January 15, 2013

MWENYEKITI WA CCM TAWI LA WASHINGTON DC AKABILIWA NA TUHUMA ZA "USAGAJI"







MWENYEKITI wa CCM, Tawi la Washington DC, Marekani, Loveness Mamuya, yupo kwenye uhasama mkali na Mtanzania mwenzake anayeishi nchini humo, Linda Bezuidenhout, kiasi cha kuchafuana na kuibua aibu nzito.

Rekodi zinaonesha kuwa Loveness na Linda walikuwa marafiki wakubwa lakini kwa sasa ni maadui wasiopikika chungu kimoja, huku mitandao ya kijamii, hususan Facebook na skendo ya usagaji, vikitajatajwa katika malumbano yao.
Baada ya malumbano na kuchafuana, wiki iliyopita mwandishi wetu aliwapata mahasimu hao, akarekodi sauti zao ambapo kila mmoja alitoa ya moyoni kuhusu mwenzake.

ALICHOKISEMA LINDA
Linda ambaye ni dada wa mshindi wa Big Brother Africa mwaka 2007, Richard Bezuidenhout alidai: “Tatizo kubwa la Loveness ni usagaji. Miaka saba iliyopita wakati naishi Maryland (Marekani), nilikuwa na matatizo ya nyumba. Nilikuwa sina hati za kuniwezesha kupanga nyumba yangu mwenyewe.


“Nikawa nachangia nyumba na watu wa nchi nyingine, nanyanyasika, tunagombana. Loveness akasikia matatizo yangu, akanipigia simu. Akaniambia ananijua tangu nikiwa Dar es Salaam. Baadaye akanishawishi nihamie kwake halafu atanisaidia kupata hati niweze kupata nyumba niishi mwenyewe na watoto wangu. Wakati huo nilikuwa na watoto wawili, mmoja ana miaka sita, mwingine mmoja na nusu.


“Nilipohamia nyumbani kwake, siku zikawa zinakwenda hafuatilii makaratasi yangu wala hataki kujishughulisha kunitafutia nyumba. Kinyume chake akawa ananitongoza tusagane, mimi nikamkatalia, basi akawa ananifuata chumbani usiku, ananilazimisha tufanye huo mchezo wa kusagana.


“Kila siku alikuja chumbani kwangu, mimi nikawa nashindwa kumjibu kwa ukali kwa kuhofia atanifukuza, nikawa nasingizia watoto wangu hawajalala, yeye anasema wamelala, mimi naendelea kumsisitizia hawajalala kwa sababu mimi ndiye nawajua.


“Siku zikawa zinakwenda, siku moja nikamuuliza ni kwa nini hataki kunisaidia kupata nyumba, au mpaka anifanyie huo mchezo? Hapo nikawa nimemtibua lakini baadaye ikabidi nijifanye nimelainika, akatulia lakini nikaendelea kumkatalia kijanja kunifanyia huo mchezo wake.


“Kuna wakati alinunua mpaka nyeti bandia ya kiume akidhani mimi nitakubali. Vilevile kuna siku alinibaka, hiyo siku siku alinunua pombe tukalewa, nilipolala, katikati ya usingizi nikashtuka kusikia mtu amenilalia.


“Nikamsukuma, kutokana na pombe sikumzingatia, nikaendelea kulala. Asubuhi nikakumbuka lile tukio, nikamuuliza Loveness kama alikuja chumbani kwangu usiku, akanijibu ndiyo na nilimsukuma. Akaniambia pia kwamba hakutaka kuendelea kwa sababu aliponishika aligundua nilikuwa katika siku mbaya.


“Nikajua mambo yamekuwa mazito, kwa hiyo nikamuomba anisaidie kupata nyumba, baada ya hapo, atakuwa anakuja kwangu tunafanya huo mchezo kwa kujiachia. Kusikia hivyo, Loveness akaondoka na mume wake, wakaenda kutafuta nyumba, jioni wakaniambia wamepata.


“Yaani baada ya kumuahidi tutakuwa tunafanya mchezo wake ndiyo akapata nyumba haraka. Nikahamia na watoto wangu. Baada ya hapo, nikamhamishia na mdogo wangu mwingine. Loveness akaona mdogo wangu atakuwa anamfanya asifanikiwe lengo lake la kufanya mchezo wa usagaji na mimi.


“Loveness akanigombanisha na mdogo wangu, akahama lakini baadaye yule mdogo wangu akaja kunipa siri nzima ya maneno ya uchonganishi aliyokuwa anaambiwa na Loveness. 


Kwa kweli kitendo cha kunigombanisha na mdogo wangu kiliniudhi sana, ikabidi nianike uchafu wote na njama zake za kujidai ananisaidia ili anifanyie mchezo wa usagaji.”

LOVENESS NAYE AKAZUNGUMZA

 
“Mimi Linda alikuwa rafiki yangu, alibadilika tu kwa sababu ya kunionea wivu. Ni uongo mtupu,” alisema Loveness na kuongeza:


“Kiukweli tuligombana kwa vitu tofauti. Alikuwa anaishi kwangu nikamfukuza kutokana na tabia zake lakini nashangaa haya mambo yamekua makubwa hivi sasa.”


WAWILI WAZIKWA HAI JIJINI MBEYA....

 Kamanda wa polisi mkoani Mbeya Diwani Athuman
 
WAKAZI wawili wa Kijiji cha Karungu, Kata ya Ivuna, Wilaya ya Momba, mkoani Mbeya wamefariki dunia baada ya kufukiwa wakiwa hai katika kaburi moja na marehemu wanaodaiwa kumuua, tukio linalohusishwa na imani za kishirikina.


Watu hao, Ernest Molela anayekadiriwa kuwa na umri zaidi ya miaka 60 na Bibi Mizinala Nachela ambaye umri wake unakadiriwa kuwa zaidi ya miaka 50, walizikwa wakiwa hai pamoja na aliyekuwa mkazi wa kijiji hicho, marehemu Nongwa Hussein.

Kaimu Ofisa Mtendaji wa Kata ya Ivuna, Joseph Silwimba aliwaambia  wanahabari jana kuwa, tukio hilo lilitokea juzi kati ya saa tano na sita mchana, muda mfupi kabla ya maziko ya Hussein.

Kabla ya kufukiwa katika kaburi moja na marehemu, Molela na Nachela kwa nyakati tofauti walipigwa hadi kuzirai na watu wanaodaiwa kushiriki kuchimba kaburi kwa ajili ya kumzika marehemu Hussein.

Silwimba alisema Hussein alifariki dunia Jumamosi saa 10 jioni baada ya kuugua kwa muda mrefu, lakini inaonekana kuwa baadhi ya wakazi wa kijiji hicho walihusisha ugonjwa huo ambao ulisababisha kifo chake na ushirikina.

Jana mchana, Mkuu wa Polisi wa Wilaya (OCD), Momba aliyefahamika kwa jina la Wendo aliongoza operesheni ya kufukua kaburi walimozikwa watu hao, ambao walikutwa wakiwa wameshafariki dunia.

Silwimba alisema miili ya Molela na Nachela ilifanyiwa uchunguzi, kisha kukabidhiwa kwa ndugu na jamaa zao ambao waliifanyia mazishi jana mchana.
Mkasa wenyewe
Kundi la vijana tisa ambao wanadaiwa kuwa ndiyo waliokuwa wakichimba kaburi la marehemu Hussein walianza msako katika Kijiji cha Karungu wakiwatafuta wale waliowatuhumu kwamba ni wachawi na kwamba walihusika na kifo chake.

Silwimba alisema katika harakati zao, walikwenda nyumbani kwa George Hussein ambaye ni kaka wa marehemu lakini hawakumkuta, hivyo kuamua kuchoma moto nyumba yake kwa kuwa walikuwa wakimtuhumu kuhusika na kifo hicho.

“Baada ya kufanya uharibifu huo, walikwenda hadi nyumbani kwa Mzee Molela kisha wakamkamata na kumpiga sana hadi hali yake ikawa mbaya kisha wakambeba hadi eneo la maziko,” alisema na kuongeza:

“Waliporejea kwenye msiba walimkuta Mama Nachela naye wakamkamata na kuanza kumpiga hadi akazimia na yeye pamoja na Molela waliwavuta hadi kwenye kaburi ambako mazishi ya Nongwa (Hussein) yalifanyika.”

Alisema baada ya jeneza kushushwa kaburini, vijana hao wanaodaiwa kwamba walikuwa na hasira walimvuta Molela na kumwamuru kuweka udongo kaburini, lakini alishindwa kufanya hivyo kutokana na hali yake kuwa mbaya.

“Baada ya kushindwa walimsukumiza kaburini na baadaye walimvuta yule mama (Nachela) ambaye naye alikuwa hajitambui na kumtupa ndani ya kaburi halafu wakawafukia wote, kisha wakaondoka,” alisema Kaimu Ofisa Mtendaji huyo.

WEMA SEPETU AJIKUTA AKIWAKUMBATIA WAZEE AKIKWEPA KUGUSWA NA "PANZI"

KATIKA hali isiyo ya kawaida ya kutozoea maisha ya kijijini, msanii asiyeishiwa matukio, Wema Sepetu, hivi karibuni alijikuta kwenye wakati mgumu baada ya kuwakumbutia wazee wa kijijini akikwepa panzi  pindi walipokuwa katika ziara ya uzinduzi wa mpango wa Kilimo Kwanza kwa vijana eneo la Kwandelo, Kondoa.


Wakati wakiwa katika harakati za kuhamasisha kilimo kwanza , panzi alianza kuruka ruka eneo hilo ambalo ni sehemu ya shamba hali iliyomchanganya msanii huyo na kuanza kukimbia hovyo huku akijifunika usoni na mkoba wake akikimbilia sehemu waliyokuwa wamesimama wazee.


Hata hivyo baada ya kurejea Dar mwandishi wetua  alizungumza na mrembo huyo ambaye  alisema kuwa hakuwai kumuona mdudu huyo hivyo hali hiyo ilimpa wasiwasi mkubwa kwa kuhisi anaweza kudhuliwa afya yake

MBATIA ANUSURIKA KUUAWA MTWARA

MBATIA ANUSURIKA KUUAWA MTWARA

Saturday, January 12, 2013

MATOKEO YA MTIHANI WA TAIFA KIDATO CHA PILI 201...

MATOKEO YA MTIHANI WA TAIFA KIDATO CHA PILI 201...:   Naibu waziri wa Elimu Philip Mulugo ametangaza matokeo ya kidato cha pili kupitia vyombo vya habari leo na yalikuwa kama ifuatavyo ...

Friday, January 11, 2013

Connect; Mombasa Raha Positions: Part 1 Of 3.

Connect; Mombasa Raha KUTOKA KENYA WANATOA MAFUNZO HAYA

Default Mwigulu Nchemba: CHADEMA itakufa 2015


Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Mwigulu Nchemba

CHAMA Cha Mapinduzi kimekitabiria kifo Chadema baada ya uchaguzi wa 2015 kikieleza kuwa CCM ikishinda, chama hicho kitakuwa hakina nguvu tena kwa kuwa Katibu Mkuu wake, Dk Willibrod Slaa atakuwa amechoka.


Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Mwigulu Nchemba aliliambia gazeti hili jana kuwa chama hicho kinapoteza umaarufu kadri siku zinavyokwenda hasa kutokana na siasa zake za uchochezi na mwaka 2015 ndio itakuwa mwisho wa chama hicho.


Alisema kitakufa na kitasahaulika kabisa, akisema sasa hivi vijana wameshaanza kuwakimbia, na kwamba anaamini pia baada ya 2015 hakuna diwani ambaye atagombea kupitia chama hicho.


Alisema pia ni mwaka ambao Katibu wa Chadema Willibrod Slaa amestaafu kwa kuwa alishatangaza asiposhinda atastaafu na Chadema haiwezi kushinda hivyo mwisho wa Dk Slaa ndio utakuwa umefika kwa kuwa nyota yake haitang’aa tena.


“Nguvu ya Dk Slaa aliyokuwa nayo miaka miwili iliyopita sio aliyonayo sasa na mpaka mwaka 2015 atakuwa ameisha kabisa.” alisisitiza.


Pia Mwigulu aliyataka makundi yaliyojichomoza ndani ya CCM ikiwa ni harakati za kuwania urais mwaka 2015 kuheshimu ilani ya chama hicho kwa kuitekeleza na kuisimamia kwa kutoleta vurugu ndani ya chama wala kujenga chuki kwa wale ambao hawawaungi mkono.


|”CCM ina utaratibu wake wa kupata mgombea na hatumzuii mtu kugombea, sisi kama kamati ya utendaji tunatekeleza maagizo aliyotoa mwenyekiti tutayasimamia kwa nguvu zote anayetaka kugombea ahakikishe havurugi chama na asitengeneze chuki kwa ambao hawamuungi mkono.”


Wakati huohuo Naibu Katibu huyo wa CCM na Mbunge wa Iramba Mashariki aliwataka wakazi wa Mtwara kuachana na propaganda zinazoenezwa na wapinzani kuhusu rasilimali ya gesi na badala yake wafanye kazi kwa maendeleo yao na taifa kwa ujumla.


“Rasilimali iliyopo ni ya taifa na watafaidika, hakuna rasilimali ya wilaya fulani, bomba la gesi ni lazima lijengwe tutawaelimisha wakazi wa Mtwara, kwani hata Ziwa Victoria bomba lilijengwa kwenda Shinyanga badala ya Kwimba, kwa nini basi halikujengwa kwenda Kwimba wakati pale ni karibu zaidi.


“Utajiri unategemea na jitihada, wasitegemee kwa vile tuna rasilimali ya gesi basi wakae wategemee watapata utajiri bila ya kufanya kazi haiwezekani, wasisubiri kupewa vya bure, ni kama mikoa yenye madini halafu wakazi wa pale wategemee Serikali itawapa vocha za kuweka kwenye simu kwa vile madini yao kwao, haiwezekani ni lazima wafanye kazi.

Source: Mwananchi

ibu Jamani-Huu ndio Uchafu Ulio Tawala ndoa Nyingi za Leo





Kama mtu  ana akili nzuri naamini  atakuwa ni mwerevu. Nawasihi wanawake  muache tabia  ya  AIBU.Muulize kinachomsibu mumeo.

Kama unaogopa kumwambia basi unaweza kumwanzisha tu pole pole wakati wa mnafanya mapenzi. Mwambie leo nataka unishike hapa. Leo tujaribu staili hii, napenda ukifanya hivi, usiwe unakuja mapema...Dear uko bize mno, naomba uwe unanijali na tufanye mara kwa mara...


Wanaume ni kama watoto wadogo na ukiwa mjanja unaweza kumbadilisha unavyotaka hasa katika mambo ya mapenzi...Vinginevyo  utakuwa ni mtu  wa  kuibiwa kila leo.


Hata huko nje utapata mume wa mtu. Mwanzoni mambo yatakuwa moto lakini baadaye mtazoeana na mambo yatakuwa yale yale.


Halafu kama ni mume wa mtu na anafanya nje  ya ndoa , unajuaje kama hana mnyororo wa wanawake huko nje?. Mmoja tu akiwa na UKIMWI kwenye huo mnyororo basi kila memba wa huo mnyororo anaishia kuudaka....