Saturday, March 30, 2013

HIVI NDIVYO MAMBO YALIVYO ENEO LA JENGO LILILOPOEROMOKA LEO



Hivi ndivyo lionekanavyo jengo hilo mara baada ya kuporomoka na asubuhi ya leo na kupelekea watu kadhaa kufukiwa na kifusi hicho wakiwepo watoto waliokuwa wakicheza mpira jirani na jengo hilo.
Watu wengi wakiwemo ndugu wa watu waliokuwepo kwenye jengo hilo wakiangalia hata ya kuokolewa kwa ndugu zao.
Juhudi za uokoaji zikiendelea japo kuna uhaba mkubwa sana wa vifaa vya uokoaji.
Moja ya Magreda yaliopo eneo hilo la tukio likiendelea na kazi  ya kutoa kifusi ili kurahisisha kazi ya uokoaji.
Kikukweli hali bado ni tete katika uokoani,maaka pia kuna ufinyu wa nafasi.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Mh. Said Meck Sadick akiwasili eneo la tukio ili kuungana na waokoaji wengine kwenye zoezi hilo.
Watu wanajitahidi kwenye uokoani,lakini kuna uhaba wa vifaa vya uokoaji.
Mkuu wa Mkoa akisogea eneo la tukio.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Mh. Mh. Said Meck Sadick akipatiwa maelezo ya namna ya uokoaji kutoka kwa maafisa wa kikosi cha Uokoaji.
Wanajitahidi lakini wanakwamishwa na vifaa.
Wadau wakionyesha nondo zilizokuwa zimejengewa kwenye jengo hilo wakimaanisha kuwa hazina ubora.
Magari yaliyokuwepo jirani na jengo hilo yakiwa yameangukiwa na kifusi.
Kazi ikiendelea huku wengine wakiwa hawaani kilichotokea.
Mawasiliano ya hapa na pale yakiendelea kuhakikisha utaratibu wa uokoaji unafanikiwa.


Kikosi ya Msalaba mwekundu kipo eneo la tukio.
Ulinzi mkali.
Mdau akiwahisha ngazi kwa ajili ya kuendeleza zoezi zima la uokoaji.

Mpiga picha wa Magazeti ya Serikali ya Daily & Sunday News na Habari leo,Mohamed Mambo akiwajibika kuhakikisha anapata picha bora.
Kumbukumbu ikichukuliwa.


Mh. James Mbatia akijadiliana jambo na mmoja wa wadau walipo eneo la tukio.

No comments: