Thursday, March 28, 2013

Lori laacha njia, laua watu wawili na kujeruhi saba Ilala, Dar

WATU wawili wamekufa papo hapo na wengine saba kujeruhiwa baada ya kugongwa na lori lililoacha njia, Wilaya ya Ilala. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Marietha Minangi alisema ajali hiyo ilitokea juzi saa 5:15 usiku katika Barabara ya Mandela eneo la Tabata Relini.
Kamanda Minangi alisema gari lenye namba za usajili T855 ATB aina ya Scania iliyokuwa ikiendeshwa na mtu asiyefahamika, akitoka Ubungo au Buguruni alipofika maeneo hayo gari hilo liliacha njia na kuwagonga watembea kwa miguu na magari mengine manne. …read more
Source: HabariLeo

No comments: