Tuesday, April 30, 2013

KUTOKA BUNGENI - KAMBI YA UPINZANI YAMCHANA KINANA


Waziri wa Mmbo ya Ndani ya Nchi-Tanzania, Dk Emmanuel Nchimbi akishambulia Upinzani wakati akichangia mjadala wa kupitisha makadirio na matumizi ya Wizara ya Maliasili na Utalii kwa mwaka wa fedha 2013/14 mjini Dodoma LEO. Dodoma, Tanzania. Kambi ya Upinzani kupitia kwa Msemaji  Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Mchungaji Peter Msigwa (Chadema), LEO ‘amemchana’ Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulharaman Kinana kwamba amekuwa akishiriki kikamilifu kufanya biashara ya pembe za ndovu zenye uzito wa tani nne.

Msigwa katika hutuba yake aliyosoma bungeni Leo amesema kwamba pembe hizo ziliripotiwa kukamatwa nchini Tanzania na Kenya mwaka 2009 na vyombo vya usalama vya Vietnam na kwamba pembe hizo zilisafishwa na kampuni ya wakala ya Sharaf Shipping Co. Ltd.

“Taarifa za Wakala wa Usajili wa Biashara na Makampuni (BRELA) zinaonyesha kwamba Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana anamiliki robo tatu ya hisa za Sharaf Shipping Co. Ltd., wakati robo iliyobaki ya hisa hizo inamilikiwa na mtu aitwaye Rahma Hussein. Kwa mujibu wa taarifa ilizonazo Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Rahma Hussein ni mkewe Abdulrahman Kinana.


“Sio tu kwamba kampuni ya Katibu Mkuu wa CCM na mkewe imehusishwa na usafirishaji haramu wa pembe za ndovu kutoka Tanzania, kampuni hiyo inaelekea kutoa
ajira haramu kwa wageni. Wakati shehena ya meno hayo tembo inakamatwa nchini Vietnam, nyaraka zilizoambatana na shehena hiyo zilionyesha kwamba kibali cha
kusafirisha shehena hiyo kilisainiwa na raia wa India anayeitwa Samir Hemani mnamo tarehe 13 Novemba 2008. Hemani alikuwa Meneja wa Fedha na Utawala wa
Sharaf Shipping Co. Ltd.
"Hata hivyo, nyaraka za Idara ya Uhamiaji ambazo Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni imezipata zinaonyesha kwamba wakati Hemani anasaini
kibali cha kusafirisha shehena ya meno ya tembo kwa niaba ya wateja wa Kinana na mkewe, kibali chake cha kuishi Tanzania kilikuwa kimeisha tangu tarehe 7
Mei, 2008,” amesema Msingwa ambaye ni Waziri Kivuli wa Wizara ya Maliasili na Utalii,  wakati LEO akiwasilisha Bungeni makadirio ya matumizi kwa mwaka wa
fedha 2013/2014.

Waziri Nchimbi Aishukia Chadema Bungeni

Wakati Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi akichangia mjadala wa kupitisha makadirio na matumizi ya Wizara ya Maliasili na Utalii kwa mwaka
wa fedha 2013/14 mjini Dodoma, ameishambulia kambi ya upinzani bungeni ikiwamo Chadema kwamba ni waongo na ameshangwa na kaili iliyotolewa na Msingwa.

Waziri Nchimbi ameishukia Chadema kueleza kwamba hoja zilizojengwa dhidi ya Katibu Mkuu wa CCM, Kinana na msemaji wa upinzani (Msigwa) kwamba Kinana
anasafisha biashara ya pembe za ndovu nje ya nchi ni uongo mtupu.

“Nimejaribu kufuatilia kwa makini alichokisema alikimaanisha, alikielewa, alikitafakari au aliandikiwa tu akaenda kusoma, baada ya kutafakari kwa kina
nikagundua hakuwa na nia mbaya, aliandikiwa tu na ameenda kusoma,” amesema Dk Nchimb

No comments: